Waambie wasijaribu, acha sie tusio na namna tutumie pikipiki,, bajaji nazo zinakuja speed kusababissha vifo na ulemavu wa kudumuInasikitisha sana. Nina rafiki zangu wana hii michezo kujidai wana haraka wanaacha magari wote washawahi kukoswakoswa na israili
Ni kweli kabisa.Kwa kutazama tu picha, hapo mtu wa boda ni lazima alikuwa anaovertake na hakuchukua taadhari...
Unaona kabisa lorry limejaribu kutoka kushoto lakini boda kwa kupanic akaenda kujibamiza...
Kwa uchunguzi wangu 90% ni abiria.
Madereva wana namna nyingi za kukwepa majanga kwa hiyo abiria ukiona boda wako anavunja sheria ukamchekea shauri yako, yakitokea ya kutokea unaenda weweKwa uchunguzi wangu 90% ni abiria.
Nchi ngumu hii, mwenye akili ndio tahira na asiyenaaakili ndio kiongozi wake na tahira.Na abiria wanao-tolerate upuuzi wa dereva wa bodaboda nao ni kundi gani? Unakuta mtu kavaa suti bodaboda inajichoneka katikati ya malori abiria anakenua meno tu kama zuzu! Mwingine unakuta yupo busy anachat kwenye simu!$%#@%^&*
Pikipiki imemuua kijana mmoja jirani wiki 2 zilizopita, kaacha mke na watoto 4,, kadogo kakiwa ni kachanga ka wiki 2 tu, mke alizaa kwa oparesheni,, yani hata machozi yawe mbali vipi ungelia tu, nililia kwa kuwaza mambo mengi, nilimuhurumia mwanamke,,, ooooh God kwanini unaruhudu haya jamani
Kanuni muhimu:Wengine tunapanda sio Kwamba tunapenda ni shida tu
Boda ni kama wametengeneza utaratibu tofauti wa kuendesha vyobo vya moto. Wengi hawafuati sheria, na hawana mpango huo.View attachment 3692058
Kwa sàsa hivi vifo vya vijana kutokana na ajali za bodaboda ni vingi mno.
Vijana wanaendesha pikipiki bila kuwa na leseni na wakati mwingi hata bila kuwa na pikipiki hizo kusajiliwa.
Vijana huwa wala hawana helmet na wabapakia wenzao wawili au watatu zsidi, naarufu kama mishkaki.
Picha hiyo hapo juu ni leo, mshikaki ulioua vijana watatu.
Hii maarufu ya mshikaki, dereva hana leseni, abiria wawili zaidi, ameovertake kwa fujo na kakutana na Howo, tani 30, huko Tanga.
Hapo maisha yakatoweka.
Bodaboda zipigwe
Pia ni kundi la kimkakati wakati wa kampeni za uchaguzi.Viongozi wasioona mbali ndio wamewaletea wananchi jinamizi la bodaboda na wala hawana mpango wa kudhibiti wingi wake...
Viongozi wameshahalalisha kuwa ni ajira rasmi na waendesha boda hawagusiki tena sababu wanaonekana kama ni kundi kubwa la wapiga kura...
Miaka mingi ijayo huko barabarani kutakuwa vurugu mechi kama ilivyo India, Indonesia au Vietnam, ambapo hizo nduzi ni nyingi kuzidi motokaa...
DuhNi kweli kabisa.
Mimi nilimgonga bodaboda aliyekuwa anenda spidi ya ngiri, katika kulikwepa dimbwi la maji upande wake akaniingia kisawaswa upande wangu wa kulia.
Nina gari la mjerumani very old model, pikipiki iliishia pale pale kama chombo cha usafiri, ilisawanyika.
Dereva alirushwa kwenye bonnet, kioo cha mbele, na akajikuta yuko juu ya gari, na mwishowe hadi nyuma ya gari.
Mikasimama kwenda kumtazama , nikashukuru Mungu bado anapumua lakini ulimi kaumeza na anashindwa kupumua vizuri na hajitambui.
Nikajua huyu asipopumua vizuri dakika tano tu anakufa.
Nikautoa ulimi kwa kidole, na haraka watu sasa wakajaa.
Akapata fahamu baada ya muda na akachukuliwakwenda hospitali.
Kwa maaumivu aliyokuwa nayo kumbe mikono yote miwili na mbavu moja imevunjika.
Alipopata fahamu kitandani akaulizwa na polisi:
Kazi hana
Leseni hana
Alikuwa amelewa
Pikipiki kaazima
Nikajua nimepigwa.
Hao ndio boda wa kwetu.
Ni tatizo kubwa sana, kila mwaka tunapoteza nguvu kazi ya taifa sababu ya pikipiki, kiasi sasa haitushtui tena hali ni mbaya na serikali ni kama haioniViongozi wasioona mbali ndio wamewaletea wananchi jinamizi la bodaboda na wala hawana mpango wa kudhibiti wingi wake...
Viongozi wameshahalalisha kuwa ni ajira rasmi na waendesha boda hawagusiki tena sababu wanaonekana kama ni kundi kubwa la wapiga kura...
Miaka mingi ijayo huko barabarani kutakuwa vurugu mechi kama ilivyo India, Indonesia au Vietnam, ambapo hizo nduzi ni nyingi kuzidi motokaa...
Kuna boda akawa anakuja kuovertake kushoto kwa fujo, nikampelekea bodi, hizo breki zikaniacha nacheka,Kuovertake kushoto hii kitu inanikera sana.
Mkuu vunjikamguu kwanza ndio utaona faida za boda!Kama ni ajali ajali zinataokea hata kwa magari,na sababu za ajali ZIPO nyingi ikiwemo changamoto za barabara n.k,
lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuwalaumu bodaboda FAIDA za boda boda na bajaji ni nyingi kuliko hizo issue za ajali,..kwanza idadi ya boda boda ni nyingi na hivyo hata ajali kuwa nyingi zinaendana na idadi ya boda zilizopo.
Mkuu vunjikamguu kwanza ndio utaona faida za boda!
Ndio maana unaambiwa panda bodaboda upate unachostahili!Kwa sababu vyombo vya usafiri Huwa vinapata ajali haimaanishi TUACHE kuvitumia,..kuna namna ya HEKIMA na BUSARA na KUTUMIA AKILI kama tunazo,ili kupunguza changamoto za vyombo vya usafiri,sio boda peke yake ajali ni kwa vyombo vyote vya usafiri.
Kutatua changamoto kwa kuzikimbia kuzira sio kutatua tatizo.