Bodi Ya Ligi imetoa maelezo marefu yasiyokuwa na maana wala misingi yoyote ya kikanuni

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
2,507
Reaction score
4,943
Nimeshangazwa na maelezo kutoka Bodi ya ligi (TPLB) kuhusu sababu ya kuahirisha mchezo, Nimegundua nguvu kubwa inayotumika na bodi kujisafisha na kujitoa makosa yake.

Sababu za kuahirishwa mchezo zinazotajwa na TPLB ni za kiusalama kwa mujibu wa maelezo yao, Kwamba kamati ya saa 72 iliahirisha mchezo kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa miongozo ya CAF na FIFA na hata katika kanuni za Ligi yetu, Kamati ya saa 72 haina mandate na uwezo wa kudadavua masuala ya kiusalama. Mambo ambayo yanaweza kuwa tishio la kiusalama zinazoweza kupelekea mechi kuahirishwa ni kama tishio la ugaidi, uwepo wa silaha za maangamizi, vita, mapinduzi ya kijeshi yanapotokea katika nchi husika nk. Na taarifa hizi hutolewa kwa barua kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika na kutoa wito kwa TPLB kuahirisha kusanyiko la watu.

Katika hayo yote utagundua TPLB hawana mamlaka ya kung'amua masuala ya kiusalama, Pia sababu zingine zinazotajwa kama rushwa hazipo kwenye miongozo na kanuni za CAF na FIFA kuwa sababu za kuahirisha mchezo, bali uchunguzi hufanyika baada ya mchezo.

Utakumbuka baadhi ya matukio yaliyosemekana kutishia amani katika dimba la Mkapa, mfano katika derby iliyopita shabiki maarufu wa Simba GB64 alisema endapo Simba ingefungwa wangeleta vurugu, Taarifa ilitolewa vyombo husika vya usalama sio na bodi/kamati ya saa 72, Tena mhusika alidhibitiwa na mchezo ukachezwa.

Kwa hayo machache itoshe kusema
TPLB ijitathmini kama inastahili kuendelea kuwepo.
 
Mbona hujanukuu hiyo Miongozo ya FIFA na CAF unayodai imetaja mambo yanayosababisha mechi iahirishwe ili na sisi wengine tuipitie?
 
Nimenukuu kwa mifano hapo, sababu za kiusalama ni kama vita, tishio la kigaidi nk. Ambapo TPLB/kamati ya saa 72 haina mamlaka nayo bali vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika hutoa taarifa kwa barua rasmi.
 
Taja vifungu hivyo vya FIFA na CAF ili sisi wengine tuvisome pia.
 
Nimenukuu kwa mifano hapo, sababu za kiusalama ni kama vita, tishio la kigaidi nk. Ambapo TPLB/kamati ya saa 72 haina mamlaka nayo bali vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika hutoa taarifa kwa barua rasmi.
Isome kanuni ya 34 yote, inasema wazi mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya hizi,elewa maana ya neno "yoyote" Hayo maelezo yako ya ugaidi umeyapata wapi?
 
Attachments

  • Screenshot_20250318-100402.png
    Screenshot_20250318-100402.png
    247 KB · Views: 31
Isome kanuni ya 34 yote, inasema wazi mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya hizi,elewa maana ya neno "yoyote" Hayo maelezo yako ya ugaidi umeyapata wapi?
Unakuwa mjinga mjinga, mara ya kwanza nimenukuu vyote, ukasema kipengele kimoja, nimenukuu hicho kipengele kimoja bado unasema "yoyote kati ya hizo" haya ebu tueleze specifically ni kanuni ipi iliyotumika? Au kukurahisishia ni sababu gani iliyopelekea mchezo kuahirishwa kwa mujibu wa kanuni?
 
Wewe ni kilaza, husomi taarifa na kuelewa,unasoma vile vipengele unavyopenda, nimenukuu kanuni yote ya 34, kanuni inasema sababu yoyote kati ya hizo,kwa uelewa wako mdogo unadhani ni sababu zote lazima zitokee ndio mchezo uahirishwe, kanuni 34:1(1.3) inawapa mamlaka,na hakuna sehemu wanalazimika kuitajja hiyo dharura,Kanuni inasema tu "sababu ya dharura itakayokubaliwa na TFF, Sababu walizotaja ni za kiusalama zimekubaliwa na TFF Wewe na vilaza wenzako endeleeni kusubiri point 3 za dezo kama mlivyosubiri goli lenu la Mamelod.Vipi bado mnatembea na mkataba wa Kagoma?
 
Katika hayo yote utagundua TPLB hawana mamlaka ya kung'amua masuala ya kiusalama, Pia sababu zingine zinazotajwa kama rushwa hazipo kwenye miongozo na kanuni za CAF na FIFA kuwa sababu za kuahirisha mchezo, bali uchunguzi hufanyika baada ya mchezo.
Ndio maana Bodi ya Ligi waliandika hivi, baada ya kupokea Taarifa ya Usalama.

Nanukuu

“” Kwasababu Bodi ya Ligi ilipokea taarifa ya usalama kutoka kwa ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyo ambatana na tukio la club ya Simba kishindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati,Bodi ya Ligi kupitia Kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imeamua kuahirisha mchezo tajwa hapo juu””

Mwisho wa kunukuu.
 
Nimeshangazwa na maelezo kutoka Bodi ya ligi (TPLB) kuhusu sababu ya kuahirisha mchezo, Nimegundua nguvu kubwa inayotumika na bodi kujisafisha na kujitoa makosa yake.

Sababu za kuahirishwa mchezo zinazotajwa na TPLB ni za kiusalama kwa mujibu wa maelezo yao, Kwamba kamati ya saa 72 iliahirisha mchezo kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa miongozo ya CAF na FIFA na hata katika kanuni za Ligi yetu, Kamati ya saa 72 haina mandate na uwezo wa kudadavua masuala ya kiusalama. Mambo ambayo yanaweza kuwa tishio la kiusalama zinazoweza kupelekea mechi kuahirishwa ni kama tishio la ugaidi, uwepo wa silaha za maangamizi, vita, mapinduzi ya kijeshi yanapotokea katika nchi husika nk. Na taarifa hizi hutolewa kwa barua kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika na kutoa wito kwa TPLB kuahirisha kusanyiko la watu.

Katika hayo yote utagundua TPLB hawana mamlaka ya kung'amua masuala ya kiusalama, Pia sababu zingine zinazotajwa kama rushwa hazipo kwenye miongozo na kanuni za CAF na FIFA kuwa sababu za kuahirisha mchezo, bali uchunguzi hufanyika baada ya mchezo.

Utakumbuka baadhi ya matukio yaliyosemekana kutishia amani katika dimba la Mkapa, mfano katika derby iliyopita shabiki maarufu wa Simba GB64 alisema endapo Simba ingefungwa wangeleta vurugu, Taarifa ilitolewa vyombo husika vya usalama sio na bodi/kamati ya saa 72, Tena mhusika alidhibitiwa na mchezo ukachezwa.

Kwa hayo machache itoshe kusema
TPLB ijitathmini kama inastahili kuendelea kuwepo.
Mkuu umemaliza Kila kitu ambae ajakuelewa atakuwa na utindio wa ubongo!
 
Wewe ni kilaza, husomi taarifa na kuelewa,unasoma vile vipengele unavyopenda, nimenukuu kanuni yote ya, kanuni inasema sababu yoyote kati ya hizo,kwa uelewa wako mdogo unadhani ni sababu zote lazima zitokee ndio mchezo uahirishwe, kanuni 34:1(1.3) inawapa mamlaka,na hakuna sehemu wanalazimika kuitajja hiyo dharura,Kanuni inasema tu "sababu ya dharura itakayokubaliwa na TFF, Sababu walizotaja ni za kiusalama zimekubaliwa na TFF Wewe na vilaza wenzako endeleeni kusubiri point 3 za dezo kama mlivyosubiri goli lenu la Mamelod.Vipi bado mnatembea na mkataba wa Kagoma?
Sababu za kiusalama za dharura zitazokubaliwa na tff sio kama hizo ilizotaja bodi kama unavyojiaminisha,,sababu za kiusalama za dharura usidhani Kila sababu inakubalika kikanuni na Sheria za fifa zinazoongoza Mpira wa miguu
Uwezi kuamka tu ukatengeneza upuuzi wako alafu ukasema ndio sababu za kiusalama zilizopelekea mechi kuahirishwa!
 
Mkuu umemaliza Kila kitu ambae ajakuelewa atakuwa na utindio wa ubongo!
Ameandika anazunguka tu.

hapo amegusia kuwa Bodi ya ligi haina uwezo wa kun’gamua matukio ya kiusalama zaidi ya vyombo vya usalama, hapo sahihi kabisa
Na Bodi ya Ligi wanasema walipewa ukiachana na taarifa barua ya Simba walipokea pia Taarifa kutoka ofisa usalama.
 
Hiyo Bodi itakuwa imejaa vilaza wasiojitambua. Maana wametumiwa na mbumbumbu kutusababishia hasara, baada ya kuogopa kushushiwa mvua ya magoli.
 
Mmeshindwa kuwashushia Tabora mvua ya magoli ndio mje kuishushia Simba iliyo nafasi ya pili na iliyowafunga 5-0 ambazo hamjawahi kuzilipa hadi sasa?
 
Ameandika anazunguka tu.

hapo amegusia kuwa Bodi ya ligi haina uwezo wa kun’gamua matukio ya kiusalama zaidi ya vyombo vya usalama, hapo sahihi kabisa
Na Bodi ya Ligi wanasema walipewa ukiachana na taarifa barua ya Simba walipokea pia Taarifa kutoka ofisa usalama.
Ni tukio Gani kubwa ambalo ni la kiusalama vyombo vya Dola vilishindwa kutoa taarifa kwa umma kama kawaida yao? Umepewa mfano wa yule shabiki wa Simba aliyetishia kufanya vurugu na vyombo vya Dola vikamuwajibisha na Mpira Ukachezwa,,itakuwaje usalama wa raia uwe shakani alafu vyombo vya Dola visitoe ripoti kwa umma?
 
Wapi pameandikwa kuwa tukio linatakiwa liwe kubwa ndiyo mechi iahirishwe ?

Halafu ukubwa wa tukio unapimwaje?
 
Ndio maana Bodi ya Ligi waliandika hivi, baada ya kupokea Taarifa ya Usalama.

Nanukuu

“” Kwasababu Bodi ya Ligi ilipokea taarifa ya usalama kutoka kwa ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyo ambatana na tukio la club ya Simba kishindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati,Bodi ya Ligi kupitia Kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imeamua kuahirisha mchezo tajwa hapo juu””

Mwisho wa kunukuu.
Ofisa usalama wa mchezo, Sio Jeshi la polisi, Sio jeshi la wananchi, hana maamuzi ya kiusalama wa nchi na tukio husika, Taarifa ilitakiwa kutolewa na jeshi husika mfano pale GB64 alipoitisha mgomo tuliona jeshi la polisi lilidhibiti kwa kumkamata na mchezo ukachezwa na 5imba akafungwa vizuri tu na mashabiki wakatawanyika makwao kwa amani. Tukiacha suala la wahusika wanaosimamia ulinzi na usalama, Je tukio gani lililoonekana kuwa tishio la kiusalama? 5imba kugomewa kufanya mazoezi? Jukumu la vyombo vya usalama ni kudhibiti na kuhakikisha usalama katika mchezo kama walivyofanya kwa GB64 sio kuahirisha mchezo! Kazi ya vyombo vya ulinzi ni ipi? Unless kama kulikuwa na tishio la kigaidi au mauaji makubwa. Tofauti na hapo Bodi haina mamlaka kuahirisha mchezo
 
Wewe ni kilaza, husomi taarifa na kuelewa,unasoma vile vipengele unavyopenda, nimenukuu kanuni yote ya 34, kanuni inasema sababu yoyote kati ya hizo,kwa uelewa wako mdogo unadhani ni sababu zote lazima zitokee ndio mchezo uahirishwe, kanuni 34:1(1.3) inawapa mamlaka,na hakuna sehemu wanalazimika kuitajja hiyo dharura,Kanuni inasema tu "sababu ya dharura itakayokubaliwa na TFF, Sababu walizotaja ni za kiusalama zimekubaliwa na TFF Wewe na vilaza wenzako endeleeni kusubiri point 3 za dezo kama mlivyosubiri goli lenu la Mamelod.Vipi bado mnatembea na mkataba wa Kagoma?
Ona ulivyo mjinga mjinga, Ulianza kutaja vipengele vyote nikachambua kipengele kimoja kimoja, unadhani ninamaanisha lazima vyote vitokee! La hasha! Hapo nakuonyesha kwamba katika hivyo vipengele hakuna hata kimoja ambacho kinahalalisha ujinga wa TPLB
 
Wapi pameandikwa kuwa tukio linatakiwa liwe kubwa ndiyo mechi iahirishwe ?

Halafu ukubwa wa tukio unapimwaje?
Wewe akuna unachokielewa tutaangaishana tu hapa,,kwaiyo wewe kwa uelewa wako tu mdogo Kila jambo likitokea mechi inaahirishwa?
Ikiwa ivyo Mpira utachezwa? Ndio maana fifa wakaweka sababu za dharura zinatakiwa ziweje ili mechi iahirishwe,,sababu kama tishio la ugaidi ni Mojawapo ya sababu nzito za kiusalama zinazoweza kupelekea mechi kuahirishwa,,usidhani Kila sababu ni hoja ya msingi kuahirisha mechi ingekuwa ivyo Kila jambo lingekuwa linapelekea mechi kuahirishwa ndio maana fifa waliona ilo wakaweka vigezo vya msingi vinavyoweza kufanya mechi iondolewe!
 
Back
Top Bottom