Nimeshangazwa na maelezo kutoka Bodi ya ligi (TPLB) kuhusu sababu ya kuahirisha mchezo, Nimegundua nguvu kubwa inayotumika na bodi kujisafisha na kujitoa makosa yake.
Sababu za kuahirishwa mchezo zinazotajwa na TPLB ni za kiusalama kwa mujibu wa maelezo yao, Kwamba kamati ya saa 72 iliahirisha mchezo kutokana na sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa miongozo ya CAF na FIFA na hata katika kanuni za Ligi yetu, Kamati ya saa 72 haina mandate na uwezo wa kudadavua masuala ya kiusalama. Mambo ambayo yanaweza kuwa tishio la kiusalama zinazoweza kupelekea mechi kuahirishwa ni kama tishio la ugaidi, uwepo wa silaha za maangamizi, vita, mapinduzi ya kijeshi yanapotokea katika nchi husika nk. Na taarifa hizi hutolewa kwa barua kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika na kutoa wito kwa TPLB kuahirisha kusanyiko la watu.
Katika hayo yote utagundua TPLB hawana mamlaka ya kung'amua masuala ya kiusalama, Pia sababu zingine zinazotajwa kama rushwa hazipo kwenye miongozo na kanuni za CAF na FIFA kuwa sababu za kuahirisha mchezo, bali uchunguzi hufanyika baada ya mchezo.
Utakumbuka baadhi ya matukio yaliyosemekana kutishia amani katika dimba la Mkapa, mfano katika derby iliyopita shabiki maarufu wa Simba GB64 alisema endapo Simba ingefungwa wangeleta vurugu, Taarifa ilitolewa vyombo husika vya usalama sio na bodi/kamati ya saa 72, Tena mhusika alidhibitiwa na mchezo ukachezwa.
Kwa hayo machache itoshe kusema
TPLB ijitathmini kama inastahili kuendelea kuwepo.