Bodi Ya Ligi imetoa maelezo marefu yasiyokuwa na maana wala misingi yoyote ya kikanuni

Bodi Ya Ligi imetoa maelezo marefu yasiyokuwa na maana wala misingi yoyote ya kikanuni

Ndio maana Bodi ya Ligi waliandika hivi, baada ya kupokea Taarifa ya Usalama.

Nanukuu

“” Kwasababu Bodi ya Ligi ilipokea taarifa ya usalama kutoka kwa ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyo ambatana na tukio la club ya Simba kishindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati,Bodi ya Ligi kupitia Kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imeamua kuahirisha mchezo tajwa hapo juu””

Mwisho wa kunukuu.
Wataje haya matukio na pia waeleze kama walihakikishiwa kuwa yasingeweza kudhibitiwa siku ya mechi(kesho yake).
 
Wewe ni kilaza na hujui kusoma kanuni,kwa taarifa yako kanuni no 34:1(1.3) inaeleza sababu yoyote itakayokubaliwa na TFF,yaani hata kama bodi wakisema wameahirisha mechi kwa sababu Mangungu amefiwa na mjomba wake,TFF wakiikubali hiyo sababu basi hiyo mechi itaahirishwa.
Yaani kanuni hiyo moja isomwe peke yake na maamuzi yafanyike bila kuangalia vipengele/kanuni zingine? Sijui kama kuna kitu cha aina hiyo.
 
Taja vifungu hivyo vya FIFA na CAF ili sisi wengine tuvisome pia.
Nawewe taja kifungu kwenye kanuni za tff au fifa au caf kinachosema timu mgeni isipofanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo basi mechi hiyo iahirishwe , mkitaja hicho kifungu kesho tu uto tunaleta timu uwanjani derby ipigwe tuwakande makolo mara ya khamsa mfululizo!
 
Nimeshangazwa na maelezo kutoka Bodi ya ligi (TPLB) kuhusu sababu ya kuahirisha mchezo, Nimegundua nguvu kubwa inayotumika na bodi kujisafisha na kujitoa makosa yake.

Sababu za kuahirishwa mchezo zinazotajwa na TPLB ni za kiusalama kwa mujibu wa maelezo yao, Kwamba kamati ya saa 72 iliahirisha mchezo kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa miongozo ya CAF na FIFA na hata katika kanuni za Ligi yetu, Kamati ya saa 72 haina mandate na uwezo wa kudadavua masuala ya kiusalama. Mambo ambayo yanaweza kuwa tishio la kiusalama zinazoweza kupelekea mechi kuahirishwa ni kama tishio la ugaidi, uwepo wa silaha za maangamizi, vita, mapinduzi ya kijeshi yanapotokea katika nchi husika nk. Na taarifa hizi hutolewa kwa barua kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi husika na kutoa wito kwa TPLB kuahirisha kusanyiko la watu.

Katika hayo yote utagundua TPLB hawana mamlaka ya kung'amua masuala ya kiusalama, Pia sababu zingine zinazotajwa kama rushwa hazipo kwenye miongozo na kanuni za CAF na FIFA kuwa sababu za kuahirisha mchezo, bali uchunguzi hufanyika baada ya mchezo.

Utakumbuka baadhi ya matukio yaliyosemekana kutishia amani katika dimba la Mkapa, mfano katika derby iliyopita shabiki maarufu wa Simba GB64 alisema endapo Simba ingefungwa wangeleta vurugu, Taarifa ilitolewa vyombo husika vya usalama sio na bodi/kamati ya saa 72, Tena mhusika alidhibitiwa na mchezo ukachezwa.

Kwa hayo machache itoshe kusema
TPLB ijitathmini kama inastahili kuendelea kuwepo.
Bodi ya Ligi hamna kitu pale wapo kama sanamu, (figure heads) , mara waseme Kuna ruswhwa, Takukuru wanajibu kwamba hawajapewa taarifa ya rushwa,

Vile vile mabua ya mahindi yaliyo simama shambani ukiwa mbali litaonekana kama ni shamba la mahindi
 
Isome kanuni ya 34 yote, inasema wazi mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya hizi,elewa maana ya neno "yoyote" Hayo maelezo yako ya ugaidi umeyapata wapi?
Sasa katika sababu hizi, ni ipi ilisababisha derby ihairishwe?
 
Baada ya kupitia uzi huu naanza kuelewa hizi nukulu kuhusiana na hawa viumbe wanaoshavikia Uto: 1) Hersi... wamevimbiwa mihogo, 2) Manara.. wawili tu wana akili, 3) Luc Emayel ... manyani hawajui kitu ..
 
Back
Top Bottom