Bodi ya Ligi yakataa ombi la Simba kutumia Chamazi.

Bodi ya Ligi yakataa ombi la Simba kutumia Chamazi.

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Bodi ya Ligi TPLB, imekataa maombi ya Simba SC ya kataka kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX, kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Simba SC imeomba kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX kwa ajili ya wachezaji wao kuuzoea uwanja huo watakaoutumia kwenye mchezo wao wa marudiano ya CAF Champions League dhidi ya Power Dynamos.

Inaelezwa Bodi ya ligi TPLB imewataka Simba SC kuendelea kuutumia uwanja wa uhuru kwasababu ndio uwanja ambao wameuchagua kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani baada ya Benjamin Mkapa kuwa kwenye Ukarabati.

Simba SC lengo lao ni kuwafanya wachezaji wao wauzoee uwanja wa AZAM COMPLEX ambao watautumia oktoba mosi dhidi ya Power Dynamos.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu uwanja ukichagua hakuna kubadilisha ndio maana El Mereikh walishindwa kwenda marakesh Morocco. Kuwa mpole
Labda itakuwa hujui taratibu zikoje za kimpira

"Una uwezo kwa mechi zisizozidi 2 za ligi kuu kubadilisha uwanja tofauti na ule uliouchagua kama wa nyumbani"
 
Back
Top Bottom