Bodi ya Ligi yakataa ombi la Simba kutumia Chamazi.

Bodi ya Ligi yakataa ombi la Simba kutumia Chamazi.

Bodi ya Ligi TPLB, imekataa maombi ya Simba SC ya kataka kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX, kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Simba SC imeomba kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX kwa ajili ya wachezaji wao kuuzoea uwanja huo watakaoutumia kwenye mchezo wao wa marudiano ya CAF Champions League dhidi ya Power Dynamos.

Inaelezwa Bodi ya ligi TPLB imewataka Simba SC kuendelea kuutumia uwanja wa uhuru kwasababu ndio uwanja ambao wameuchagua kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani baada ya Benjamin Mkapa kuwa kwenye Ukarabati.

Simba SC lengo lao ni kuwafanya wachezaji wao wauzoee uwanja wa AZAM COMPLEX ambao watautumia oktoba mosi dhidi ya Power Dynamos.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanataka kuja kupandikiza minyau hapo ya kiuchawi Ili kuwakomoa Yanga...

Wabaki huko huko
 
Unabadilisha uwanja kwa sababu zipi! tena siku Moja kabla ya mechi na mpinzani wako humfikirii ..huo ni umbumbumbu

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Wapi pamesemwa kuwa Simba imeomba kubadili mechi siku moja kabla ya mechi hebu tuache ushabiki maandazi

Sio kila jambo linahitaji ushabiki tuangalie sheria pia
 
Hivi wale waliokuwa wanawapeleka Simba na Yanga, mara Mwanza, Arusha, Songea, Kigoma nk, waliruhusiwa kwa utaratibu gani?
Nadhani kulikuwa na kanuni ya kuruhusu team kuchagua atmost two matches za nyumbani kuchezwa kwenye uwanja tofauti. Na izo teams huwa zinapendekea mapema ni match gani wanataka kubadilisha uwanja

Lengo ni kuinua wigo wa mapato wa team ndogo hasa zinapokutana na team kubwa kama za kariakoo. So wanazipeleka hizi team mikoa yenye hamasa na viwanja vinavyobeba watu wengi zaidi.
 
Bodi ya Ligi TPLB, imekataa maombi ya Simba SC ya kataka kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX, kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Simba SC imeomba kuutumia uwanja wa AZAM COMPLEX kwa ajili ya wachezaji wao kuuzoea uwanja huo watakaoutumia kwenye mchezo wao wa marudiano ya CAF Champions League dhidi ya Power Dynamos.

Inaelezwa Bodi ya ligi TPLB imewataka Simba SC kuendelea kuutumia uwanja wa uhuru kwasababu ndio uwanja ambao wameuchagua kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani baada ya Benjamin Mkapa kuwa kwenye Ukarabati.

Simba SC lengo lao ni kuwafanya wachezaji wao wauzoee uwanja wa AZAM COMPLEX ambao watautumia oktoba mosi dhidi ya Power Dynamos.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kuna sababu nyingine sawa.
Ila kisingizio cha kusema walichagua mwanzo hapa maana kuna timu huwa zinapeleka mechi mikoani na zinakubaliwa
 
Mkuu uwanja ukichagua hakuna kubadilisha ndio maana El Mereikh walishindwa kwenda marakesh Morocco. Kuwa mpole
Sheria ipi hiyo??
Maana nakumbuka mwaka flani ruvu shooting alipelek mechi mwanza badala ya uwanja wa mabatini baadae akapelek nyingine arusha
 
Back
Top Bottom