Bodi ya Ligi TPLB, imekataa maombi ya Simba SC ya kataka kutumia uwanja wa AZAM COMPLEX, kwnye mchezo wao wa kesho dhidi ya Costal Union ya Tanga.
Simba SC imeomba kutumia uwanja wa AZAM COMPLEX kwa ajili ya wachezaji wao kuuzoea uwanja huo watakaoutumia kwenye mchezo wao wa marudiano ya CAF CL dhidi ya Power Dynamos.
Inaelezwa Bodi ya ligi TPLB imewataka Simba SC kuendelea kuutumia uwanja wa uhuru kwasababu ndio uwanja ambao wameuchagua kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani baada ya Benjamin Mkapa kuwa kwenye Ukarabati.
Simba SC lengo lao ni kuwafanya wachezaji wao wauzoee uwanja wa AZAM COMPLEX ambao watautumia oktoba mosi dhidi ya Power Dynamos.
Sent using
Jamii Forums mobile app