Bodi ya Maziwa kuharibu maziwa ya ng'ombe kwa kuyamwagia mafuta ya taa

Bodi ya Maziwa kuharibu maziwa ya ng'ombe kwa kuyamwagia mafuta ya taa

Maziwa ya mgando ya Tanga Fresh na Asas yanauzwa madukani yakiwa katika vifungashio vya plastic.
Iweje ndoo za plastic ziwe haramu, lakini vifungashio viwe halali?
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Wizara ya Mifugo ametangaza kwamba Waziri Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa aliyekuwa anaongoza zoezi la kumwagia mafuta ya taa kwenye maziwa kuanzia jana tarehe 26 Juni 2020.
Hujuma wanafanyiwa itakuwa

Ova
 
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
CCM kumejaa wauaji
 
Hata kichaa huwa anasema lakini asemayo ni pumba.

Hata Mbowe alisema watu wasiojulikana kumbe ni Konyagi.

Kwahiyo kusema sema wakati mwingine bila kuwaza ni sawa na ukichaa
Kanywe na wewe konyagi
 
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa ngombe katika bara la Africa baada ya Ethiopia bali maziwa mengi yanayo sindikiwa hayatokani na ngombe wa kitanzania isipokuwa yale ya ASAS na Tanga Fresh ukiacha yale ya wasindikaji wadogo wadogo.

Kama ni kweli watendaji wa Bodi ya Maziwa waliharibu maziwa yanayouzwa Ubungo na watanzania wanyonge, basi inabidi mamlaka husika iwawajibishe waliohusika na kitendo hicho cha kinyama.

Maziwa yanayo unzwa Ubungo mengi yanatoka mkoa wa Pwani na Morogoro, hususan wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo, Mororogoro na Mvomero. Maziwa haya yana zalishwa na wafugaji wadogo wadogo. Hivyo basi, jambo la muhimu la kufanya ni kutoa elimu sahihi kuhusu uhifadhi wa maziwa ili iwafikie walaji yakiwa masafi na salama na siyo kuyaharibu maziwa kwa kuwa gharama ya kuzalisha lita moja ya maziwa ni kubwa sana! Kwa mfano Bodi kwenye vikao vyake inatakiwa kukutana na wadau na kujadili changamoto zinazo wakabili wananchi walioko kwenye mnyororo wa thamani wa zao la maziwa.

Hata hivyo, moja wapo ya changamoto kubwa inayo wakabili wazalishaji wadogogo wadaogo wa maziwa na wauza maziwa n:
1.) Ukosefu wa elimu ya uhifadhi wa zao la maziwa kwa njia safi na salama.

2.) Pili ni ukosefu wa vifaa vya kupimia maziwa kama vile "strip cup" kwa ajili ya mastitis na "lactometer" inayotumika kubaini wingi wa maji kwenye maziwa.

3.) Tatu ni ukosefu wa vifaa vya aluminum vya kuhifadhia maziwa wakati yanapo safirishwa.

4.) Nne ni ukosefu wa matengi makubwa "cooling collection centres" ili kuendelea kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu yasiharinike na kuendelea kuwa na ubora wake.

Kwa mtizamo wangu mimi pamoja na mambo mengine haya ndiyo yalikuwa majukumu ya msingi kusimamiwa na Bodi ya Maziwa na siyo vinginevyo. Tukishapunguza mapungufu yaliyo bainishwa hapo basi tuendelee kufuatilia kuhakikisha kuwa zao la maziwa lina mfikia mlaji wa mwisho yakiwa safi na salama.
 
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
Ukatili uliije[emoji28]
 
Kufungu Cha sheria kinasema maziwa yauzwe au yatunzwe kwenye chombo Cha Aluminium, Sasa pia kila sheria huwa ineeleza kushindwa kutekeleza hivyo au kufanya kinyume na sheria tajwa adhabu yake Ni ......je Sheria hii ya utunzaji maziwa ktk chombo Cha Aluminium ikikiukwa adhabu yake Ni ipi?? Au ndiyo hiyo ya kumwamgia mafuta ya taa na Rangi?? Pia mwenyekiti wa bodi hii utakuta kaandika barua ya kuomba fedha ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kumwamgia maziwa pale ubungo na mhasibu ama mtunza fedha ama mkurugenzi wa bodi akaidhinisha manunuzi hayo!!!!
 
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
Hii nchi ina mambo Mengi sana ya kipumbavu...huyu mtendaji kwa sababu yeye anapokea mshahara na marupurupu anachukulia mambo kirahisi sana..
Nitafurahi sana ikiwa Mh Rais ataiona hii na kushughulika nae ni mtu mnyama sana fala huyu....hana huruma
 
Maziwa ya mgando ya Tanga Fresh na Asas yanauzwa madukani yakiwa katika vifungashio vya plastic.
Iweje ndoo za plastic ziwe haramu, lakini vifungashio viwe halali?
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Wizara ya Mifugo ametangaza kwamba Waziri Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa aliyekuwa anaongoza zoezi la kumwagia mafuta ya taa kwenye maziwa kuanzia jana tarehe 26 Juni 2020.
Huyu shetani hakupaswa kutenguliwa tu alipaswa hata kufungwa
 
Hujuma wanafanyiwa itakuwa

Ova
Ndoo za plastic hazitakiwi beba maziwa kutoka point A kwenda B sababu bado hayajachakatwa. Pia uoshaji wa plastic sio kama Aluminium cans.
 
Watoe taarifa inayoeleweka na ufanunuzi yakinifu wananchi waweze kuwaelewa.

Kwamba maziwa yakiuziwa kwrnye ndoo za plastic yana madhara gani kwa binadamu? Siyo kutoa tu marufuku, watanzania wote waelewe!

Na kama kuna madhara mbona vifungashio vya hayo maziwa ni plastic na vimejaa kwenye Supermarkets na mafuka mengi tu ya rejareja? Je, TFDA wanalijua hilo na wanapita kwenye hzo supermarkets?

Kama kuna madhara basi Watanzania wengi sana watakuwa wamedhurika!!
TFDA walishafariki, siku hizi ni TBS anafanya hiyo kazi. Shida kubwa ya Tanzania ni unafiki na kujipendekeza kuonekana wapo kazini, au kuna mtu ana kiosk chake hawataki hao wa mama hapo.
Arusha nzima ni gallons za plastic zinasambaza Maziwa na hakuna hatua inayochukuliwa.

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Juzi walisema wanazuia maziwa ya nje ya unga ili wakulima wa ndani wapate solo..Leo wanamwagia mafuta ya taa maziwa ya wakulima wanyonge wa ndani..hiyo case Kuna mtu ataliwa kichwa...mbona super market maziwa yanauzwa kwenye ndoo za plastic na vifuko vya lailoni au kwakuwa hao wamama hawauzii supermarket.
 
wakimwagia mafuta ya Taa ndo yanarudi kwenye Ubora?
Uwe wasoma kuliko kukurupuka.
Maziwa yakipelekwa viwandani yakikutwa hayajakidhi viwango huwekewa rangi au mafuta ili usiyauze tena. Hivyo bodi nayo ikaona ifanye hivyo
 
[QUOTE="mwarobaini_, post: 35826044, member: 583346".
Kwanza uwepo tu wa hiyo bodi ya maziwa ni uendawazimu uliotukuka.
[/QUOTE]
Naam, kwa uzoefu wangu mdogo, mazao mengi ya kilimo yaliyo undiwa bodi ufanisi wake huwa unaharibiwa.
 
Back
Top Bottom