ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.
Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.
Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa ngombe katika bara la Africa baada ya Ethiopia bali maziwa mengi yanayo sindikiwa hayatokani na ngombe wa kitanzania isipokuwa yale ya ASAS na Tanga Fresh ukiacha yale ya wasindikaji wadogo wadogo.
Kama ni kweli watendaji wa Bodi ya Maziwa waliharibu maziwa yanayouzwa Ubungo na watanzania wanyonge, basi inabidi mamlaka husika iwawajibishe waliohusika na kitendo hicho cha kinyama.
Maziwa yanayo unzwa Ubungo mengi yanatoka mkoa wa Pwani na Morogoro, hususan wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo, Mororogoro na Mvomero. Maziwa haya yana zalishwa na wafugaji wadogo wadogo. Hivyo basi, jambo la muhimu la kufanya ni kutoa elimu sahihi kuhusu uhifadhi wa maziwa ili iwafikie walaji yakiwa masafi na salama na siyo kuyaharibu maziwa kwa kuwa gharama ya kuzalisha lita moja ya maziwa ni kubwa sana! Kwa mfano Bodi kwenye vikao vyake inatakiwa kukutana na wadau na kujadili changamoto zinazo wakabili wananchi walioko kwenye mnyororo wa thamani wa zao la maziwa.
Hata hivyo, moja wapo ya changamoto kubwa inayo wakabili wazalishaji wadogogo wadaogo wa maziwa na wauza maziwa n:
1.) Ukosefu wa elimu ya uhifadhi wa zao la maziwa kwa njia safi na salama.
2.) Pili ni ukosefu wa vifaa vya kupimia maziwa kama vile "strip cup" kwa ajili ya mastitis na "lactometer" inayotumika kubaini wingi wa maji kwenye maziwa.
3.) Tatu ni ukosefu wa vifaa vya aluminum vya kuhifadhia maziwa wakati yanapo safirishwa.
4.) Nne ni ukosefu wa matengi makubwa "cooling collection centres" ili kuendelea kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu yasiharinike na kuendelea kuwa na ubora wake.
Kwa mtizamo wangu mimi pamoja na mambo mengine haya ndiyo yalikuwa majukumu ya msingi kusimamiwa na Bodi ya Maziwa na siyo vinginevyo. Tukishapunguza mapungufu yaliyo bainishwa hapo basi tuendelee kufuatilia kuhakikisha kuwa zao la maziwa lina mfikia mlaji wa mwisho yakiwa safi na salama.