Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (HESLB) kumtumia control namba mtu asiye na ajira ni kumuongezea stress, badilikeni!

Hapana yani nilitaka kujau kama wanatafta namba za watu maana watu wengi bila shaka wanabadili namba. Mimi nimemaliza kabla ya usajili wa namba kwa vitambulisho vya nida. Nimemaliza kabla ya vitambulisho la nida so kubadili namba ilikuwa sana tu ndo maana nimeuliza.
Kuhusu kulipa fedha, mimi naona serikali iache kulipisha watu maana ina fedha nyingi za kunua magari, kulipa wenza wa viongozi, kupeleka wasanii nje lakini si kusomesha watu wake bure. Iweke tu vigezo fulani vya ufaulu watu wapate mikopo bure.
Kwanza itafanya watu wasome sana ili kushindania kupata freee education.
 
Ukiwapa KAZI lini Ili upate uhalali wa kuwadai?

Hapo ukute una miaka zaidi ya 60 lakini Bado ni mtumishi wa Serikali.

Ruto ameshavunja Baraza la mawaziri Kwa shinikizo la Hawa Hawa mnaowadharau.
Andamaneni, vijana wa Tanganyika kofia na Flana zinawatosha.
SOMA HAPO SHERIA YA BODI, wapi wamesema utatafutiwa kazi ili ulipe?

19.-(1) It shall be the duty of every loan beneficiary under this Act torepay his debt to the Government through the Board.
(2) The debt that the loan beneficiary shall be liable to repay to theGovernment under subsection
(1), shall be the total sum of money-
(a) calculated on the basis of student loan agreement;
(b) which shall be established as a fact by the Board as havingreceived by him personally and or through his banka ccount; and

.
 
ELIMU ni ya thamani, Si vyema kuwa Bure.

Muhimu hapo ufanye KAZI upate pesa Kisha ulipe Kwa furaha bila kufuatwa fuatwa.
 
Sasa watalipaje bila kuwa na KAZI yenye kuingiza pesa ya kutosha kulipa?

Unaonaje ukiomba msaada wa jeshi likusaidie kuwaminya watu Hawa wasio na KAZI walipe hizo ml 16 wanazodaiwa Kila Mmoja?πŸ€”
 
Sasa watalipaje bila kuwa na KAZI yenye kuingiza pesa ya kutosha kulipa?

Unaonaje ukiomba msaada wa jeshi likusaidie kuwaminya watu Hawa wasio na KAZI walipe hizo ml 16 wanazodaiwa Kila Mmoja?πŸ€”
Mkuu mtu kama hajavaa kiatu chako hawezi akakuelewa unachomaanisha ,Inasikitisha sana watu wanakuja na facts zao za ajabu , sema maisha ni haya haya πŸ™
 
Sasa watalipaje bila kuwa na KAZI yenye kuingiza pesa ya kutosha kulipa?

Unaonaje ukiomba msaada wa jeshi likusaidie kuwaminya watu Hawa wasio na KAZI walipe hizo ml 16 wanazodaiwa Kila Mmoja?πŸ€”
Mwanangu, hilo swali ilibidi kabla ya kuomba mkopo uwaambie kuwa hutalipa bila kazi ili wasikupe.
Kumbe tunalaumu serikali kuhusu ufisadi ila SISI WANANCHI ni mafisadi namba 1.
 
Mkuu mtu kama hajavaa kiatu chako hawezi akakuelewa unachomaanisha ,Inasikitisha sana watu wanakuja na facts zao za ajabu , sema maisha ni haya haya πŸ™
Nina HAKIKA tungekuwa live ana Kwa ana,

Angeficha Ujinga wake kuepuka Aibu na fedheha Kwa reaction Kutoka Kwa umma!!
 
Mwanangu, hilo swali ilibidi kabla ya kuomba mkopo uwaambie kuwa hutalipa bila kazi ili wasikupe.
Kumbe tunalaumu serikali kuhusu ufisadi ila SISI WANANCHI ni mafisadi namba 1.
Si kutolipa mkopo pekee,

HAKI ya kwanza ya binadamu, ni HAKI ya kuishi.

Serikali Inatakiwa iwape wananchi wasio na ajira posho ya kujikimu Ili wapate HAKI hiyo muhimu,

Wakiona hawawezi kuwapa pesa ya kula, basi wawatengenezee ajira.

Anyway, nikuulize, ikiwa mkopeshaji anajua hakuna uhakika wa kulipwa sababu hakuna ajira, anakopesha Ili iweje?
 
A Hahahaha wamekuwa kausha damu hii nchi ya hovyo sana
 
1. Sasa, waambie chama tawala kitunge sera, zipelekwe bungeni , zipitishwe na itungwe sheria, hakuna shida na si tamko kama unavyofikiri.

2. Mpewe ruzuku wakati mda wote mnakesha vibanda vya kubeti mkikuna nywele za ndani na ku-like picha za kina diamond na Mbosso!

3. Unaacha mashamba bikra huko Itilima, Mbozi na Kigozela unakuja Dar kukesha vijiwe vya pweza ?
 
Wakizingatia wazo hili hakika tutafika mbali
 
Vitu vingine vinatia hasira mno.
 
Wamekusikia.
 
Pole sana..
Ila Dawa Ya Deni Ni Kulipa...
 
Sawa pesa mkopo lazima kulipwa, lakini sio kwa namna hiyo. Imekaa kienyeji sana kudai hivyo. Ni kama wamepaniki yani. Sijui ni nani anatoa mawazo ya namna hii.
.
 
Sawa pesa mkopo lazima kulipwa, lakini sio kwa namna hiyo. Imekaa kienyeji sana kudai hivyo. Ni kama wamepaniki yani. Sijui ni nani anatoa mawazo ya namna hii.
.
Ni nani mwingine kama sio mtunza kibubu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…