Salaam, shalom!!!
Ninapata malalamiko mengi Kwa vijana wangu wengi Walio mtaani wanaopambana kujitafuta Ili wapate chochote kitu Cha kujikimu mahitaji Yao na ya wanaowategemea.
HESLB, bodi ya mikopo, unapomkopesha mwanafunzi wa chuo, lazima unakuwa na taarifa zake, namba ya simu IPO, namba ya nida , nk nk.
Na Kwa kawaida, mtu huyo akipata KAZI serikalini au sekta binafsi, taarifa zake zikipelekwa NSSF, PSPF,nk lazima mtajua kuwa mtu huyo tayari ameingia mfumo wa kupata pesa, hapo ni sawa kumpigia simu au kuwasiliana na waajiri wake Ili kupata namna Bora ya Kupata mkopo mliomkopesha.
Sasa, kumtumia controll namba kwamba mnamdai M. 16, yaani 16,000,000/= kijana aliyemaliza chuo, hajapata KAZI, Hana hata mia, aliyebomolewa Banda lake la biashara na mgambo wa Jiji,wengine wanarandaranda wakifanya vibarua mtaani, ghafula inaingia message yenye ujumbe ulioambatana na bill ya control namba yenye kuonyesha deni analodaiwa na bodi ya mikopo HESLB, hamuoni kuwa Hali hiyo ni kumuongezea stress?
USHAURI.
1. Bodi ya mikopo, HESLB, kupata pesa yenu kirahisi, wasiliana na Waziri Mwigulu Nchemba na waziri wa Ajira Ili mshauriane, ipatikane namna Bora ya kuwaajiri Hawa vijana Kwa namna mbalimbali Ili pesa ya umma iweze kurudi Kwa wakati.
2. Hakikisheni mifumo inasomana, kama kijana hajaajiriwa mnatakiwa kujua Ili kuepuka usumbufu na stress mnazowasababishia Hawa vijana.
3. TRA, Wizara ya Fedha, viwanda na biashara, Ajira, shirikianeni Ili kusaidia vijana Hawa wafungue kampuni, walelewe na kupata msamaha wa Kodi Ili wakuze biashara zao, waongeze tax base na walipe mikopo wanayodaiwa na bodi ya mikopo HESLB na waweze pia kulipa Kodi Ili kukuza Uchumi wa Nchi.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Karibuni 🙏. Cc:
mwigulu nchemba
PIA SOMA
-
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu