The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Ni takribani miaka 20 sasa tangu mwaka 2004 ambapo Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) ilianzishwa na imekuwa ikitegemewa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kuelekea vyuo vikuu. Licha kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi lakini bado imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanafunzi kutokana na kutoa kiwango kidogo cha fedha hasa ada ambayo haiendani na ukubwa wa ada inayopaswa kulipwa chuoni hivyo kuacha mzigo mkubwa kwa wanafunzi na wazazi wao ambao wengi uwezo wa kiuchumi ni mdogo hatimaye baadhi yao kukwama kuendelea na masomo.
Bajeti bodi ya mikopo mwaka Mwaka huu 2024/25, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa TZS 284.8 bilioni. licha ya kiwango hicho cha fedha bado upangaji wa mikopo kwa wanafunzi bado hauridhishi kutokana na kiwango kidogo cha ada ambacho bodi inatoa huku wengine wakikosa kabisa.
Kuna namna nahisi bodi wanaona wakitoa fedha za kujikimu ambazo kwa kiwango kikubwa wanafunzi wengi wanapata (boom) wanaona kama wamemaliza lakini wanasahau kuwa kuna mzigo mkubwa kwenye kipengele cha ada mpaka kuna wakati wanafunzi wanazuiliwa kufanya mitihani kutokana na kushindwa kulipa ada.
Kwa kweli mimi siridhishwi na kiwango cha ada ambacho bodi ya mikopo inatoa kwa wanafunzi wetu wa vyuo vikuu, utaratibu wa upangaji wao wa mikopo kwenye kipengele cha ada (Tuition fee) uangaliwe upya.