Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu HESLB imetimiza miaka 20, je imekuwa msaada ipavyo kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo kufikia elimu ya juu?

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Ni takribani miaka 20 sasa tangu mwaka 2004 ambapo Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) ilianzishwa na imekuwa ikitegemewa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kuelekea vyuo vikuu. Licha kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi lakini bado imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanafunzi kutokana na kutoa kiwango kidogo cha fedha hasa ada ambayo haiendani na ukubwa wa ada inayopaswa kulipwa chuoni hivyo kuacha mzigo mkubwa kwa wanafunzi na wazazi wao ambao wengi uwezo wa kiuchumi ni mdogo hatimaye baadhi yao kukwama kuendelea na masomo.

Bajeti bodi ya mikopo mwaka Mwaka huu 2024/25, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa TZS 284.8 bilioni. licha ya kiwango hicho cha fedha bado upangaji wa mikopo kwa wanafunzi bado hauridhishi kutokana na kiwango kidogo cha ada ambacho bodi inatoa huku wengine wakikosa kabisa.

Kuna namna nahisi bodi wanaona wakitoa fedha za kujikimu ambazo kwa kiwango kikubwa wanafunzi wengi wanapata (boom) wanaona kama wamemaliza lakini wanasahau kuwa kuna mzigo mkubwa kwenye kipengele cha ada mpaka kuna wakati wanafunzi wanazuiliwa kufanya mitihani kutokana na kushindwa kulipa ada.

Kwa kweli mimi siridhishwi na kiwango cha ada ambacho bodi ya mikopo inatoa kwa wanafunzi wetu wa vyuo vikuu, utaratibu wa upangaji wao wa mikopo kwenye kipengele cha ada (Tuition fee) uangaliwe upya.

GauMD8_WIAA3TO1.jpg
 
View attachment 3139090
upangaji wa mikopo bodi wajitathmini upya
 
Inasaidia sema tatizo ajira hakuna hivyo kukwaza urejeshaji mikopo
 
Binafsi bila choyo wala nini bila heslb nisingesoma chuo, wapewe maua yao

Nimelipiwa ada na boom kidogo nilikuwa najazia ada hongera sana kwa hawa watu.
wewe ilibahatika ukapata vizuri kwa wakati wako, wapo wanafunzi sasahivi wameshindwa kwenda chuo kutokana na kupangiwa kiasi kidogo sana cha ada au wengine kukosa kabisa
 
Japo ccm siwapendi lakini bila loans board udsm ningepasikia kwenye radio... Big up sana
 
Wanajitahidi, Wameokoa jahazi kwa tulio wengi. Ila makato ya 15% kwenye mshahara ni makubwa mno 😀
 
  • Katika ada 1,260,000 walinilipia 1,200,000
  • Walinipa boom
  • Wakanipa books & stationery
  • Mwaka wa tatu mwanzoni nilivochukua boom na books & stationery nikakacha chuo kwenda mtaani kuhustle
  • Nikakaa mwaka mzima mtaani, yalivonishinda nikaongea na wenye chuo mana niliacha bila taarifa ikabidi niandika barua ya ku postpone lakini nikai backdate ioneshe nilisimama kwa taarifa. Wakaisaini, wakanipa ya kuniruhusu na loan officer akazitumia kuambatanisha bodi... nikarudishiwa mkopo ambao waliacha kunipa baada ya kuwa sikusaini mara kadhaa
  • Mwaka ule ulivoisha nikarudi college, bodi wakanipa hela zote (hata zile ambazo nilipokea kabla sijakacha)... pamoja na ya research, nikagraduate salama.

Wengine bila bodi tusingesoma chuo.
 
Back
Top Bottom