Ungesikiliza mahojiano ya Julio na wasafi anasema wakati Simba inatakiwa kuingia kwenye uwekezaji Abubakari Bakhresa alikubaliana na viongozi wa Simba ajenge uwanja Bunju, awape bilioni 3 za usajili Kila mwaka na pia Kuna maji yangetengenezwa na kupewa jina la Simba mapato yangepatikana wangegawa. Baada ya mo kupata habari ndio akawaundia kesi kina Aveva ili awaondoe aweze kuingia.
Ukimsikiliza Kigwangala anasema Kama mo angetoa bilioni 20 zingewekwa treasure bond na Kila mwaka Simba ingepata bilioni 3 na ushee lakini mo alikataa udhamini wa Azam ambao kwa miaka 10 ungewapa bilioni 40 na akasema Simba ikiishiwa atatoa pesa zake mfukoni Sasa iweje Leo afai alikuwa anakopeshwa na ziingizwe kwenye hesabu ya bilioni 20.
Mo alisema Leo naondoka Simba haipitii nusu saa tayari mwekezaji atakuwa kapatikana
Kuna angle ambayo hujaifikiria bado.
Bakhressa alitaka kuichukua Simba lakini hiyo ni baada ya kuiona ipo katika nafasi nzuri ambayo imetengenezwa na MO.
Sasa kuna vitu ambavyo vilikuwa vikisemwa ambavyo siwezi kuvithibitisha kuwa ni kweli ila unapofufuliwa huu mjadala hatuwezi kuacha hizo hoja kuziweka ili ku connect dots.
Inasemekana kilichotokea ni kwamba Bakhressa alitoa fungu kwa baadhi ya viongozi wafanye kampeni za kumpindua MO ili yeye aingie madarakani.
Na ndio maana baada ya MO kuwasanukia akaamua kuwatimua.
Na hii kasumba ya Bakhressa kutoa rushwa ili kufanikisha adhma yake imekuwa kawaida.
Kama utakumbuka kwenye ishu ya broadcasting Bakhressa inasemekana pia alitoa hongo kubwa kwa TFF ili wasimpe nafasi Supersport ambaye alikuwa mshindani wake mkuu.
We unashawishika na hoja ya Kingwangala kuwa kuna 3B ambayo Simba ingeweza kuipata kila mwaka na kuona hiyo kama ndio pesa nyingi kuliko zile zinazotumika kutoka mfukoni mwa MO.
Una amini kuwa 3B ambayo ungekuwa unaipata kila mwaka ilikuwa ni pesa nyingi kuliko summation ya pesa zote kwa mwaka ambazo zinatumika kupitia mkono wa MO?
Kamsikikize huyo CPA alivyokuwa anaeleza Agost 23 mwaka jana. Alisema zile 20B ambazo zipo escrow zinajizalisha kila mwaka na pesa inaingia kwenye Club ila hakutaja kiwango.
Lakini pia kuna pesa nyingine nyingi za uendeshaji ambazo MO anatoa ukiachana na hiyo 20B.
Bado pesa hizo thamani yake huioni?
Halafu kitu kingine unabidi ujue changamoto ya Simba kwa sasa sio pesa ni uongozi.
Kama umewasikikiza Che Malone na Cadena utaona hawalalamiki kuhusu mishahara yao kutolipwa kwa wakati.
Wanalalamika kuhusu mfumo wa uongozi ambao ndio hao wajumbe ambao wanataka Mo aondoke.