Hospitali binafsi ziache uhuni. Kimsingi serikali yenye ndio ilianza kudekeza haya mambo baada ya wakwepa kodi wa kariakoo kutishia kufunga maduka. Ikamlazimu waziri mkuu kusimama masaa kadhaa akiwasikiliza. Wakatoa madai yaonwaendelee kukwepa kodi.
Madawa yameteremka bei kutokana na sababu mbalimbali unalazimishaje bei iwe ile ile? Mbona madawa yaliyopanda bei hawasemi. Kumwona daktari hawasemi. Zamani kuosha damu ilikuwa 500,000 leo 150,000 wanataka ibaki 500,000?.
Waacheni wasipokee wagonjwa wa NHIF. Hospitali za serikali ni nzuri sana kwa sasa. Nashangaa watu wanaenda hospitali binafsi.
Daktari yule wa hospitali binafsi anatoka hospitali ya serikali. Akifika hosp binafsi, kumeona ni mara 2 ya hosp ya serikali. Amepandaje bei wakati kichwa ni kile kile?Halafu mnalia lia tengenezeni madaktari wenu.