Mambo yote hayawezi kwenda kwa pamoja mkuu,kwa kuwa resources hazitoshi.Sijui kama unajua concept ya prioritization kweli wewe na sijui kama unajua kwamba priority yako inaweza isiwe yangu kweli.Hata hivyo tukumbuke kwamba serikali hii ipo kisheria na tumeipa mamlaka ya kutuongoza.Sasa kwa kuwa tumekubali kwamba ituongozee,ni lazima tuiache ifanye kazi.Jambo la msingi ni kwamba tunaona matumizi ya fedha yetu.Mbona serikali tatu zilizopita hazikutufanyia lolote,si afadhali hii tunaona tangible results.Mtu mmoja mmoja unaweza usikubaliane na mambo serikali inayofanya,lakini mimi naamini kwamba majority ya watu wanakubaliana na kile serikali hii inachofanya.Siku zote tukumbuke kwamba ufalme uliogawanyika hauwezi kusimama,kwa hiyo tumuunge mkono Rais kwa maendeleo chanya ya taifa letu.Tukiwa na umoja the sky will be the limit.