Utajiri mkubwa wa mafuta Nigeria lakini nchi hiyo kimaendeleo bado iko nyuma sana. Angalia UAE utajiri wa mafuta mkubwa jinsi ulivyoibadilisha nchi ile ndani ya miaka 25 tu.
Angalia Tanzania utajiri mkubwa wa rasilimali mbali mbali lakini mikataba ya kifisadi kila kukicha ambayo haina maslahi kwa Watanzania kwa miaka nenda miaka rudi.
Madini ya Tanzanet yanapatikana Tanzania tu lakini India inaongoza kwa mapato ya Tanzanet, ikifuatiwa na USA, kisha Kenya halafu ndiyo sisi! Sijui kama huu si ushithole country ni kitu gani!!!!
Dhahabu, Almasi, gesi, uranium na rasilimali nyingine chungu nzima zote hizi kwa miaka 57 ya uhuru.
Kila kitu chetu ni shakalabaghala, elimu, miundo mbinu, hospitali zetu, ajira, mishahara pamoja na utajiri mkubwa sana wa rasilimali.
Mkapa mwizi na fisadi, Kikwete mwizi na fisadi na Magufuli naye ni mwizi na fisadi na ushahidi kwa wote hawa upo wa kutosha tu kuweza kuwapandisha kizimbani lakini wahalifu hawa wanalindana miaka nenda miaka rudi huku wakijilimbikizia mali kwa njia haramu na nchi ikibaki nyuma kimaendeleo.
Huu ni mwaka wa tatu unaingia Wafanyakazi wa Serikali nchini hawana nyongeza ya mshahara, sasa wanaambiwa wasubiri eti mpaka miradi mikubwa yote ikamilike!!!! Wakati huo huo wiki chache zilizopita tuliambiwa Serikali ina pesa nyingi sana!!! Pesa ya kufanya yale yasiyo na tija kwa Taifa ipo lakini kwa nyongeza ya mishahara kwa Wafanyakazi pesa HAKUNA!!!
Sasa hivi nchi inaendeshwa kihuni huni tu! Bunge linadharauliwa, mahakama zinadharauliwa, sheria za nchi zinadharauliwa hata Viongozi wa dini nao wanadharauliwa kumbuka waraka wa Maaskofu.
Mambo ni kidikteta dikteta tu! Halafu unashangaa tukiitwa shithole countries!!!! TUJITATHMINI ILI TUBADILIKE NA KUONYESHA KWAMBA tunaweza kubadilika badala ya kuendelea kuwapigia makofi wahalifu wanaojifanya ni Viongozi.
Kuna nchi Duniani huwa inajiendesha kwa Rais wake kuzunguka Duniani kuwawakilisha?
Kwa akili yako ni lazima Rais awawakilishe wananchi kwenye mikutano?
Ni kitu gani Tanzania inakosa kwa kutowakilishwa na Rais?
View attachment 764715