Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

kashauriwa aweke 60
Inategemea na kiwanja maana kitaamua sana kwenye idadi ya cement na nondo.

Kama kiwanja kina slope kitahitaji huenda mikanda miwili na nguzo za kutosha kwa ajili ya reinforcement au underground kwenye msingi hivyo kuongeza idadi ya cement

Na ndio maana tunashauri ramani ziwe na vipimo iwe rahisi kukadiria na mtu aeleze ikiwa kiwanja ni slope au tambarare
 
Wakuu Salaam kwenu
Kwa mimi nikapanga hivi
Tofali 2500 @ 1100 = 2,750,000
cement 50 @ 16,000 = 800,000
Mchanga fiat 2 @ 150,000 = 300,000
Nondo sjapata maesab ila naiwekea 1M
Ufundi. 2,500,000

jumla ni kama 7,350,000~ 8M

Wakuu 8M boma si linaisha bila utata wowote?

Nakarbisha Maoni, critics n.kView attachment 2629226
Sijaona gharama za kokoto hapo!
Sijaona gharama za mchanga au kifusi cha kuweka level ardhi
Sijaona gharama ya kusambaza huo mchanga kila chumba kuweka level
Sijaona gharama za stage za kukodi baada ya kufika kozi ya tano
Sijaona gharama za mbao za kukodi wakati wa kufunga lenta.
Sijaona gharama ya mbao zako za kufitisha, na zile za kukatwa kuweka ndani ya zege, papi za milangoni na madirishani, mirunda ya kushikilia.
Sijaona gharama za maji kwa hatua zote za ujenzi.
Boma bila choo halijakamilika. Sijaona gharama za kuchimba shimo la choo, nondo na cement, gaharama za mafundi, mbao za kukodi au kununua kushikia zege....

Mambo bado ni mengi, ila vingine nimesahau,
 
Kujenga ni ishu bila 20M apo sitaend popot. hawa mafund sio w kuwaamin kiviile
 
tena unaeza ukabak na chench
Kama ni boma tu kwa hiyo milioni 8 upo sahihi kabisa kwa hiyo ramani kama ulipatia vile....kuna usafiri wa material na maji na mbao za kushikia msingi na lenta ila upo exactly kabisa, ila fanya mil.8.5 tu.
 
Nondo anasema kaweka 1M

Kokoto?
Mbao/Marine za zege?


Ngoja kuna vijihesabu kama.
Maji,Mixer ya zege au
Hahaha tumuonee huruma hapo mixer ya zege tusiiweke, tufanye tu wasaidizi wa mafundi watachanganya wenyewe zege ili kupunguza gharama kwa kuwa sio ghorofa ni nyumba ya kawaida tu
 
Msingi pekee unaweza ukala m5. Hidden costs ni nyingi. Kuna vitu kama kujazia kifusi, gharama za usafiri, gharama za kuchimba msingi, maji ya kununua, mirunda, mbao, misumari n.k, hujaziweka. Pia hizo tofali zinaweza zikaingia elf nne kutegemea na urefu wa msingi na ukubwa wa madarisha.
Kwa boma hili mpaka unafunga lenta, gharama zinaweza kucheza kwenye m15.
Cha muhimu wewe anza, mpaka pale nguvu itapoishia ndio ujipange tena...
 
Wakuu Salaam kwenu
Kwa mimi nikapanga hivi
Tofali 2500 @ 1100 = 2,750,000
cement 50 @ 16,000 = 800,000
Mchanga fiat 2 @ 150,000 = 300,000
Nondo sjapata maesab ila naiwekea 1M
Ufundi. 2,500,000

jumla ni kama 7,350,000~ 8M

Wakuu 8M boma si linaisha bila utata wowote?

Nakarbisha Maoni, critics n.kView attachment 2629226
Mfuko wa Cement ni sh16000 wapi kaka?
 
Huwa mimi binafsi sipendi mgeni akinitembelea na akitaka kutumia choo/bafu apite koridoni ambako anakuwa anaona/access milango ya vyumba vyote.

mfano kwa ramani yako mgeni akienda toilet anaona chumba chako master, watoto na kingine.Ramani nitakayochagu nitajitahidi kuweka public toilet mahala ambapo hatokuwa na access ya kuona milango yote ya vyumba vya kulala.


Anyway big up kwa Ramani nzuri ya nyumba.


ushauri kwa nini usingetafuta hata 150,000 ukampa Dogo wa mwaka wa nne hapo Udsm akakuchorea structural na 150,000 nyingine mpe hapo Quantity surveyor apige gharama zote ili ujue kuwa gharama zote zinarange kiasia gani walau kwa 90% Effieciency
 
Kwanini inch 6 mkuu??
Nyumba ni msingi,
Msingi ndio unobeba nyumba,
Tofali la inch 6 lina depth ambazo zinahimili kubeba uzito wa nyumba

Na ndio maana hakuna ghorofa lenye msingi wa tofali za inch 5.

Kwa mfano hata nyumba ya ghorofa moja, msingi wake na ile nyumba ya chini sikuzote huwa ni inch 6 tena zilizolazwa ili zibebe ile nyumba ya juu
 
na mm nalenga hapo chini mpaka lenta bas kwa 8M kuna mtu kasem sitobii
Tofali 2500 ni za kuinua boma (ignore roofing design). Foundation unatumia nini? Tofali 2500 zinakula mifuko ya saruji 32 roughly. 18 iliyobaki itatosha kwa foundation na zege?
 
Duuh ujenzi ungekuwa rahisi hivi kila mtu si angekuwa na nyumba, hiyo nyumba ya 8M kulingana na mahesabu yako haina mabati, mbao, misumari, kokoto, milango, madirisha bado finishing ya vikorokoro vingine au hivyo kwako ni anasa [emoji16][emoji16]
Tunazungumzia Boma tu rejea title
 
Back
Top Bottom