Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

Kwa sababu wahindi wameruhusiwa wapo huru kufanya wanavyosikia. Sio nondo tu, Square/round pipes zilikuwa 20feet sasa hadi 18feet unapata, unapata hadi zenye 0.6mm thickness mkuu wakati standard zinatakiwa walau 1mm, yaani nchi hii tabu tupu, nondo za 12mm ukipima kwa vernier calliper ni around 10.8
Hahaa inafikia wakati unashindwa kutofautisha nondo ya 12mm na 10mm

Maana ukiangalia zile diameter hazitofautiani au zimepishana kidogo sana ukipima na vernier caliper
 
True yani, mfano kuna Kamaka, FMJ na jamaa wengine wanaitwa Shananga, ukilinganisha bei zao kama ni mdau wa ujenzi utapata materials at very low cost.
Kwa mdau wa ujenzi hawa wadau ni muhimu sana kuwa na mawasiliano nao hawanaga longolongo kwenye discount
 
Usimkatishe tamaa, courage
..courage, anaihitaji sana hii ili afanye jambo.
simkatishi tamaa lakini anatakiwa kutengeneza bajeti ya kutosha ili aweze kufanikisha lengo lake.

Kuna baadhi huwa wanaambiwa utajenga kwa milioni 10 lakini anamaliza hiyo 10 hajafika po pote ndipo hapo anaanza kulalamika.
 
Yani mimi nitoe hela yangu ninunue mchanga, yani mchanga niununue kweli kabisa?, sijui matofali halafu likianguka linibonde niumie?, kwakweli siwezi aisee. Ninunue mchanga halafu nikifa huohuo uje unifukie?, jengeni tu.
 
simkatishi tamaa lakini anatakiwa kutengeneza bajeti ya kutosha ili aweze kufanikisha lengo lake.

Kuna baadhi huwa wanaambiwa utajenga kwa milioni 10 lakini anamaliza hiyo 10 hajafika po pote ndipo hapo anaanza kulalamika.
Unaongea ukweli mkuu....kule kunahitaji pesa ya kutosha
 
Mmmh haya
Ndio witty, yeye aende site na hiyo 8m mkononi, aanze na foundation....akishafunga mkanda atapata majibu kama inatosha au aongeze, ila hapo tayari msingi utakuwepo.[emoji28][emoji28]
 
Humu utatishwa unaweza ukashindwa hata kujenga,anza ujenzi itakapoishia hela ndio hapo hapo...
 
Back
Top Bottom