Bomba la mafuta EACOP toka Uganda lazima lijengwe

Mkuu 'Jidu', ni wewe umeandika haya?

Nami ninakupongeza kwa kutaka nchi yetu ipate maendeleo,... lakini hapo hapo ninakuomba /ninawaomba waTanzania na wengine wote duniani, hasa katika nchi zetu hizi maskini; tuwe makini sana kuliko tulivyowahi kuwa makini, nadiriki hata kusema, tuwe makini kuliko tulivyokuwa wakati wa kupigania uhuru wetu.

Hizi ni nyakati tofauti sana, tusipojipanga vizuri tutazidi kuporomoka.

Ninachoweza kusema sasa ni kwamba "Ogopa sana."

Nisizunguke sana kuhusu ninachotaka kukiwasilisha hapa.

Mabadiliko ya kimazingira siyo maneno matupu, ni ukweli uliothibitika.
Nchi zetu hizi maskini hazina mitaji ya kuendeleza miradi ya mali asili tulizonazo wenyewe, tunawategemea hao wakubwa ambao wao ndio hasa waliochafua mazingira kwetu sote.

Hawa wakubwa sasa wanasema hawatawekeza tena kwenye miradi inayoongeza uchafuzi wa mazingira.

Makampuni haya tunayotegemea yawekeze, kama 'Total' ni ya huko huko kwa wakubwa, ambao sasa wameelemewa na makundi yanayohimiza miradi hii isiendelezwe.
Kassim yeye atapiga kakifua kake kwa ujenzi wa bomba kwa misingi ipi?

Binafsi nigeomba tuanze kuwa watu wenye fikra pevu. Tusiwe watu wa kujigamba tu huku tukijua hatuna uwezo wa kufanya hayo tunayojigamba nayo.

Lakini niseme hivi: Kassim akija hapa na kueleza njia zetu tunazoweza kuzitumia wenyewe kufanya baadhi ya mambo yetu wenyewe bila ya kuwategemea hao wenye mitaji, nitamsikiliza kwa heshima zote.
 
Tusijidharau wajameni!
 
Tuliambiwa tukijenga bomba la mafuta la TAZAMA na reli ya TAZARA tungekuwa vizuri kiuchumi enzi hizo, lakini ndio sasa tuko kwenye tozo kila mahali,
Wanasiasa sio wa kuwaamini Mkuu
Hilo Bomba la Crude Oil ni tofauti kidogo na hili la TAZAMA.

Hilo la Crude volume itakuwa kubwa hata Wanasiasa wakiiba vipi.
 
Hilo Bomba la Crude Oil ni tofauti kidogo na hili la TAZAMA.

Hilo la Crude volume itakuwa kubwa hata Wanasiasa wakiiba vipi.
Wanasiasa hawatosheki mkuu, hivi tuna maliasili nyingi sana, utalii, madini, lakini bado tunakabana, tozo kila mahali,
Tungepata viongozi makini, nchi yetu ilistahili kupata maendeleo mazuri
 

Ulimsikia alivyosema mwenyewe, live? Kuna hata haja ya kumung'unya lolote?

"Huko ndiko kulikuwa kulilia sasa."

Hakuna aliposema lazima lijengwe ila akigombelezea ati kuwa wako tayari kutoa ushirikiano kwenye lolote wadau wetu wa maendeleo wangependa kuelewa.

Hii ngoma bado sana.
 
Wanasiasa hawatosheki mkuu, hivi tuna maliasili nyingi sana, utalii, madini, lakini bado tunakabana, tozo kila mahali,
Tungepata viongozi makini, nchi yetu ilistahili kupata maendeleo mazuri
Hili bomba la Hoima ni uzalendo kuliunga mkono no matter what, unajua wanatufikiri sisi ni Wanaijeria.

Lile bomba la kampuni ya Shell huko Nigeria limetobolewa sana na limechafua mazingira sana pale kwenye Delta ya Mto Niger.

Sisi hili tulilinde kwa kuwa kila pipa moja la Crude Oil linalopita kwenye ardhi yetu tunapata Dola.

Sema kwenye tathmini ya mashamba ya watu wasiwapunje, kama wanavyofanya hawa wa mwendokasi kuwalipa "peanuts" wananchi katka nchi yao.
 
Wenye mali ndio wataamua ambao ni Uganda na Total Wala sio PM hata angejigamba vipi hana huo uamzi wa mwisho.
Thanks.....maana naona ni kama bomba limekuwa issue Tz badala ya wenye mafuta na wamiliki halisi.......btw hivi lile bomba la mafuta kutoka Dar kwenda Zambia huwa bado lipo na huko labda tupate mrejesho na tija hadi sasa kwa Tz........
 
Tusijidharau wajameni!
Sijui una maana gani hapa, lakini kama hunijui mimi ni mtu wa mwisho kabisa kujidharau, na hali ni hivyo hivyo inapohusu taifa langu, na wengine wote tunaodharauliwa kwa kuwa na hali duni.

Lakini inaelekea hukuelewa nilichoandika hapo, nawe ukadhani ni "kujidharau".

Ninaelewa, wengi wetu hapa haya maswala ya mazingira bado hatuyaelewi vya kutosha. Na yanapochagizwa na hawa wakoloni, ndipo tunapoamsha mori na kudhani (pengine kiuhakika), kwamba ni watu wasiotutakia sisi mema.

Ndiyo, humo humo, kuna wanaotumia mwanya huu katika kutafuta mwendelezo wa hali zetu duni. Wamo wengi sana. Lakini hawa wasitupotezee lengo nasi tukakosa weledi wa kujua hatari halisi inalalia wapi. Tukijua hivyo, ni wajibu wetu kujiandaa, na kujipa ufahamu mzuri juu ya haya mambo ili tusiwe tunaburuzwa tu inapokuja katika maamuzi yanayotuhusu na yanayohusu raslimali zetu tunazotaka kuzitumia ili nasi zitukwamue, kama wao za kwao zilivyowakwamua na matiokeo ya kutumia raslimali hizo wakapata maendeleo kwa mgongo wa kuharibu mazingira kwa wote, siyo kwa wao peke yao.

Ninahimiza tufanye nini?

Kwanza, tuelewe ukweli wa hali hatarishi iliyopo duniani kutokana na uharibifu wa mazingira. Hii siyo propaganda tena, ni ukweli unaothibitishwa kisayansi. Tusibeze, kwa vile wengi wa wanaopiga kelele ni hao tunaodhani hawatutakii mema.

Pili, pamoja na kujua uharibifu wa mazingira uliopo sasa, sehemu kubwa ikiwa imesababishwa na mataifa makubwa yaliyoendelea, na ambayo sasa yanatuminya nasi tusitumie raslimali zetu kama walivyozitumia wao kujiletea maendeleo, ni wajibu wetu kufanya kila juhudi kutafuta njia za kuzitumia raslimali hizo kila inapowezekana, hasa panapokuwepo na njia za kupunguza huo uharibifu kwa kutumia teknologia mpya zilizopo.
Huu ni wajibu wetu, lakini hatuwezi kuutimiza kama kazi tunayoweza ni kupiga tu kelele kujibishana na hao wasiotutakia mema. Ni lazima tujijengee uwezo wa kuzitumia sisi wenyewe. Tuachane na hizi tabia za kulialia kila mara, kila tunabobanwa juu ya haya maswala ya mazingira.

Tatu, kama inatuwia vigumu kuchimba mkaa wetu sisi wenyewe na kuutumia kwa maendeleo yetu, na hatuwezi kupata ufadhiri kutoka nje kwa vile mkaa ni bidhaa inayochafua mazingira, inabidi sasa nasi tuwe mbele, pengine kuzidi wengine wote katika maswala ya teknologia inayohusu njia zisizokuwa za uchafuzi wa mazingira. Tusikae tu na kubweteka tukisubiri hao wengine ndio wawe watu wa kuja hapa kututengenezea vitu kwa kutumia nyenzo tulizo nazo sisi wenyewe.
Jua tunalo hapa kila siku ndani ya mwaka mzima, kwa nini ushiriki wetu katika kutumia raslimali hii aliyotupendelea Mwenyezi Mungu kuwa nayo hapa sisi wenyewe na tulazimike kuombeleza kwa hao hao tunaosema wanatunyanyasa?
Sasa kama ni "Kujidharau" katika kuhimiza haya, huku tukirudi kule kule kwa kujidhani hatuwezi chochote, hapo nitakubaliana nawe kwamba tunajidharau.

Ningependa kumwona kiongozi anayejiamini na kuamini uwezo wetu tulio nao sasa, na kama haupo, ambaye yupo tayari kuwahimiza wananchi kuwa na ujasiri huo wa kujiamini kufanya mambo yetu wenyewe. Hili halina maana kwamba tutaacha kushirikiana na wengine duniani, ili tupanue uwezo wetu haraka na zaidi.

Mkuu 'Masopa', ninakupmba sana, usiniweke tena katika kundi hilo la "kujidharau". Sina chembe hata kidogo ya sifa hiyo.

Mwisho: Nina mashaka makubwa, kama gesi yetu kule baharini kuna siku itachimbwa. Labda mambo ya Putin yazidi kuwa mazito.

Ninashukuru pia kusikia maneno juu ya Bandari yetu ya Bagamoyo. Kama yasemwayo ni kweli kuhusu kuanza kazi sisi wenyewe juu ya bandari hiyo, nitatafuta niliyowahi kuandika humu JF kuhusu kazi ya namna hiyo kuianza sisi wenyewe kukupa ushahidi kwamba mimi siyo mtu wa kujidharau, au kudharau uwezo wa wananchi wetu kufanya mambo.
Kitu pekee kinachokosekana ni uongozi wa kutuaminisha kwamba uwezo tunao mwingi sana wa kubadili hali zetu sisi wenyewe, hapahapa Tanzania.

Hukousiyo "KUJIDHARAU."
 
Kwa nini EU wanapinga? Je ni kweli kuna unyanyasaji wa haki za binadamu na kukosekana demokrasia Uganda na Tanzania?Je wachina watatusaidia?
 
Mradi ujengwe na ulindwe maana kuna jirani wetu wa kaskazini ameona wivu kupindukia na anataka kuharibu kila kitu baada ya kukosa tenda. Kwani barabara zinapojengwa watu hawahamishwi? Aidha walipwe au wasilipwe, wananchi wanatakiwa wapishe mradi. Haya ndiyo yale mambo eti ya kuonewa huruma na mbaya wako. Kama ni haya mambo ndiyo yanaendelea, je nchi yetu itaweza kufanya lolote kweli ? Kwenye maendeleo lazima watu wengine waumie kwa faida ya wengi. Hao Ulaya wameharibu nchi zao vibaya halafu wanajifanya wanatuonea huruma. UPUUZI MTUPU.
 
pia ni hatari kuzisaidia nchi zenye udikteta kukua kiuchumi
 
 
The European Parliament has criticised a proposed East African pipeline, calling for TotalEnergies to consider an alternative route.

The resolution expressed “grave concern” around alleged human rights violations in Uganda and Tanzania, linked to the Lake Albert project. The plan covers upstream investments at Tilenga and Kingfisher, with the East African Crude Oil Pipeline (EACOP) running to the Tanzanian port of Tanga.

The text said that this had led to the “wrongful imprisonment of human rights defenders, the arbitrary suspension of NGOs, arbitrary prison sentences and the eviction of hundreds of people from their land without fair and adequate compensation”.

Uganda and Tanzania should launch efforts to ensure respect and compliance for human rights.

In particular, it called for the Ugandan government to reauthorise 54 NGOs that had been “arbitrarily closed or suspended”. It also said Ugandan authorities should provide free and unhindered access to the oil zone for independent observers, from local groups to international observers.
 
Mkuu hao wakubwa wana ajenda zao za siri za kukandamizi nchi za uchumi mchanga ili ziendelee kuwa masoko ya bidhaa zao.
Leo wanatuambia gesi, mafuta ni nishati chafuzi lakini wanalia na Urusi kuwanyima gesi kwa ajili ya viwanda vyao.
Kwa kifupi hawa wenzetu si wa kuwaamini sana kama unataka kuendelea.
 
Mkuu hilo ndilo ambal yulaliunga mkono kwa taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu.
Watu wanawaamini sana hawa wenzetu kiasi cha kuwa kiguumizi katika mambo ambayo ni faida hata kwa wao wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…