masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Ningependa kkubaliana na wewe mkuu lakini naona hulioni tatizo kubwa la wenzetu, tatizo la " me first".Sijui una maana gani hapa, lakini kama hunijui mimi ni mtu wa mwisho kabisa kujidharau, na hali ni hivyo hivyo inapohusu taifa langu, na wengine wote tunaodharauliwa kwa kuwa na hali duni.
Lakini inaelekea hukuelewa nilichoandika hapo, nawe ukadhani ni "kujidharau".
Ninaelewa, wengi wetu hapa haya maswala ya mazingira bado hatuyaelewi vya kutosha. Na yanapochagizwa na hawa wakoloni, ndipo tunapoamsha mori na kudhani (pengine kiuhakika), kwamba ni watu wasiotutakia sisi mema.
Ndiyo, humo humo, kuna wanaotumia mwanya huu katika kutafuta mwendelezo wa hali zetu duni. Wamo wengi sana. Lakini hawa wasitupotezee lengo nasi tukakosa weledi wa kujua hatari halisi inalalia wapi. Tukijua hivyo, ni wajibu wetu kujiandaa, na kujipa ufahamu mzuri juu ya haya mambo ili tusiwe tunaburuzwa tu inapokuja katika maamuzi yanayotuhusu na yanayohusu raslimali zetu tunazotaka kuzitumia ili nasi zitukwamue, kama wao za kwao zilivyowakwamua na matiokeo ya kutumia raslimali hizo wakapata maendeleo kwa mgongo wa kuharibu mazingira kwa wote, siyo kwa wao peke yao.
Ninahimiza tufanye nini?
Kwanza, tuelewe ukweli wa hali hatarishi iliyopo duniani kutokana na uharibifu wa mazingira. Hii siyo propaganda tena, ni ukweli unaothibitishwa kisayansi. Tusibeze, kwa vile wengi wa wanaopiga kelele ni hao tunaodhani hawatutakii mema.
Pili, pamoja na kujua uharibifu wa mazingira uliopo sasa, sehemu kubwa ikiwa imesababishwa na mataifa makubwa yaliyoendelea, na ambayo sasa yanatuminya nasi tusitumie raslimali zetu kama walivyozitumia wao kujiletea maendeleo, ni wajibu wetu kufanya kila juhudi kutafuta njia za kuzitumia raslimali hizo kila inapowezekana, hasa panapokuwepo na njia za kupunguza huo uharibifu kwa kutumia teknologia mpya zilizopo.
Huu ni wajibu wetu, lakini hatuwezi kuutimiza kama kazi tunayoweza ni kupiga tu kelele kujibishana na hao wasiotutakia mema. Ni lazima tujijengee uwezo wa kuzitumia sisi wenyewe. Tuachane na hizi tabia za kulialia kila mara, kila tunabobanwa juu ya haya maswala ya mazingira.
Tatu, kama inatuwia vigumu kuchimba mkaa wetu sisi wenyewe na kuutumia kwa maendeleo yetu, na hatuwezi kupata ufadhiri kutoka nje kwa vile mkaa ni bidhaa inayochafua mazingira, inabidi sasa nasi tuwe mbele, pengine kuzidi wengine wote katika maswala ya teknologia inayohusu njia zisizokuwa za uchafuzi wa mazingira. Tusikae tu na kubweteka tukisubiri hao wengine ndio wawe watu wa kuja hapa kututengenezea vitu kwa kutumia nyenzo tulizo nazo sisi wenyewe.
Jua tunalo hapa kila siku ndani ya mwaka mzima, kwa nini ushiriki wetu katika kutumia raslimali hii aliyotupendelea Mwenyezi Mungu kuwa nayo hapa sisi wenyewe na tulazimike kuombeleza kwa hao hao tunaosema wanatunyanyasa?
Sasa kama ni "Kujidharau" katika kuhimiza haya, huku tukirudi kule kule kwa kujidhani hatuwezi chochote, hapo nitakubaliana nawe kwamba tunajidharau.
Ningependa kumwona kiongozi anayejiamini na kuamini uwezo wetu tulio nao sasa, na kama haupo, ambaye yupo tayari kuwahimiza wananchi kuwa na ujasiri huo wa kujiamini kufanya mambo yetu wenyewe. Hili halina maana kwamba tutaacha kushirikiana na wengine duniani, ili tupanue uwezo wetu haraka na zaidi.
Mkuu 'Masopa', ninakupmba sana, usiniweke tena katika kundi hilo la "kujidharau". Sina chembe hata kidogo ya sifa hiyo.
Mwisho: Nina mashaka makubwa, kama gesi yetu kule baharini kuna siku itachimbwa. Labda mambo ya Putin yazidi kuwa mazito.
Ninashukuru pia kusikia maneno juu ya Bandari yetu ya Bagamoyo. Kama yasemwayo ni kweli kuhusu kuanza kazi sisi wenyewe juu ya bandari hiyo, nitatafuta niliyowahi kuandika humu JF kuhusu kazi ya namna hiyo kuianza sisi wenyewe kukupa ushahidi kwamba mimi siyo mtu wa kujidharau, au kudharau uwezo wa wananchi wetu kufanya mambo.
Kitu pekee kinachokosekana ni uongozi wa kutuaminisha kwamba uwezo tunao mwingi sana wa kubadili hali zetu sisi wenyewe, hapahapa Tanzania.
Hukousiyo "KUJIDHARAU."
Wenzetu wana tabia isiyoisha ya kujifikiria kwanza kuliko kitu kingine chochote.
Kwa tatizo la mazingira, uchumi za nchi zao zimechangia kwa zaidi ya asilimia 75 wakati sisi hatuchangii matatizo ya mazingira kwa hata asilimia 2 dunia nzima.
Wazo la kusitisha miradi yetu ya maendeleo lingekuwa na mantki kama wao wangekuwa wa kwanza kusitisha matumizi ya nishati zilizopo.
Hatujasahau kuwa hata mradi wa Umeme wa Rufiji, JNHHP waliukosoa na kukataa kuukopesha kwa vigezo hivyo hivyo.
KIFUPI, hawa wenzetu hawatutakii mema na tukiendelea kuwasikiliza tutaendelea kuwa tegemezi daima dumu.
Na ndio maana tamko la Waziri Mkuu lazima liungwe mkono.