Bomba la mafuta EACOP toka Uganda lazima lijengwe

Ningependa kkubaliana na wewe mkuu lakini naona hulioni tatizo kubwa la wenzetu, tatizo la " me first".
Wenzetu wana tabia isiyoisha ya kujifikiria kwanza kuliko kitu kingine chochote.

Kwa tatizo la mazingira, uchumi za nchi zao zimechangia kwa zaidi ya asilimia 75 wakati sisi hatuchangii matatizo ya mazingira kwa hata asilimia 2 dunia nzima.

Wazo la kusitisha miradi yetu ya maendeleo lingekuwa na mantki kama wao wangekuwa wa kwanza kusitisha matumizi ya nishati zilizopo.
Hatujasahau kuwa hata mradi wa Umeme wa Rufiji, JNHHP waliukosoa na kukataa kuukopesha kwa vigezo hivyo hivyo.
KIFUPI, hawa wenzetu hawatutakii mema na tukiendelea kuwasikiliza tutaendelea kuwa tegemezi daima dumu.
Na ndio maana tamko la Waziri Mkuu lazima liungwe mkono.
 
Mkuu toa codes japo kiduchu ya hao EU you wawili wadhamini wa ISS
 
Sijui nisemeje hapa ili nieleweke vizuri.

Haya unayosema hapa ni kweli kabisa na hayana pingamizi kwangu hata kidogo.

Hawa siyo watu wanaotutakia mema. Siyo watu wanaotaka tuwe huru, bila ya kuwategemea wao.Siku zote wanatafuta njia za wao kutuweka chini ya 'influence' yao, tuwasikilize wao wanasema nini, na kila maamuzi tunayofanya kwanza yawafikie wao na kuyaridhia. Huu ndio msukumo unaotawala maamuzi yao juu yetu.

Sasa, baada ya kusema hayo, naomba unielewe ninaposimamia.

Ni kwamba sisi wenyewe katika matendo yetu tunajiweka kuwa daima chini ya himaya yao. Hatuamini kwamba nasi tunaweza kufanya juhudi za kujinasua ili kila mara tusiwe watu wa kuwakimbilia hawa wakubwa na kuwategemea kwa mambo hata yaliyo chini ya uwezo wetu.
Wao walipokuwa wanachafua mazingira wakati wa ujenzi wa chumi zao hawakukimbilia kwetu kuja kuuliza wafanye nini; kwa sababu walihangaika wenyewe kutafuta njia za kujinasua na umaskini wa nchi zao.

Tofauti na sisi,kila jambo dogo ni kutegemea wao na wala hatuonyeshi makasiriko tunaposimangwa kama wanavyofanya sasa hivi, kwa nini?
Ni sisi wenyewe tunajiweka katika hali duni ya kiutegemezi kwao, ndiyo maana hawaoni aibu kabisa ya kutudharau kama watoto.

Miaka zaidi ya 60, baada ya kupata fursa ya kujiamlia mambo yetu wenyewe, bado tunaonekana kama watoto wadogo? Tutakuwa wakubwa lini?

Kabla sijaondoka hapa, ngoja nikupe mfano dhahiri kabisa unaoendana na mradi huu wa EACOP, unaotufanya tuwe kama watoto na hawa washenzi kutudharau kama wanvyofanya sasa.
Haya maswala ya "Uchafuzi wa Mazingira", na mambo ya "Haki za Binaadam", kwa nini yawe mambo magumu sana kwetu kuyatimiza bila hata kutumiwa kama fimbo ya kutupigia na hao wakubwa?

Kuna ugumu gani wa kueleza/kudadavua yote yanavyohitajiwa kwenye mradi husika na kuyaweka wazi kwa kila anayetaka kujua ajue? Kwa nini tufanye mambo yetu kizembezembe na kuficha au kutotoa taarifa kamilifu?

Hawa wapumbavu wanatumia mianya ya uzembe wetu na kutufanya tuonekane kama hatuna akili.

Kama kuna watu wanaotakiwa kuhamishwa kupisha mradi, kuna ugumu gani wa kuonyesha hatua zote zilizotumika na makubaliano na hao raia wetu hadi wakakubali kujengewa nyumba kwa mfano? Badala yake, sisi tunazuga tu, nyumba zilizojengwa hazionekani, inakuwa kama stori tu!

Ni mambo ya uzembe kama haya, kutotaka kufanya mambo yetu katika tratibu ndiyo yanayoleta maudhi, na kuwaruhusu hawa washenzi kutunyanyasa. Na yapo mengi sana ya aina hii yanayotufanya tuonekane kama majuha.
 
Cassim ndio nani bwashee?
 
Ningependa kkubaliana na wewe mkuu lakini naona hulioni tatizo kubwa la wenzetu, tatizo la " me first".
Wenzetu wana tabia isiyoisha ya kujifikiria kwanza kuliko kitu kingine chochote.
Katika hili sina tofauti yoyote na wewe.

Lakini wakati huo huo nasi inalazimu tukubali kwamba tunachangia katika kufanya hao watuone katika mwonekano huo.
Hili ndilo tatizo kwetu. 'Mentality' hii nayo, utaanza kuona tunapewa heshima tunayostahiri kupewa.

Tena hawana hata aibu wanapoonyesha waziwazi kutopenda sisi tujikwamue toka kwenye utegemezi kwao.

Sasa kuhusu hilo unaloita "...wazo la waziri mkuu", shida yangu ndipo hapo inapoanzia.
Tumuunge mkono kwa kitu gani, kwa kupiga kelele bila ya kufanya lolote kutuwezesha sisi wenyewe kukataa kunyanyaswa?
Tuunge mkono kitu gani, "kulalamika"?

Kesho Waziri Mkuu akitoka na kutoa hotuba inayotoa mwongozo/dira ya kulifanya taifa la Tanzania kujitambua na kuanza juhudi za kujiondoa kwenye manyanyaso haya, nami utanisikia nikiunga mkono Waziri Mkuu wangu.
Hapa sioni chochote cha kuunga mkono.

Hao Total Energies, ambao ni kampuni raia wa huko wanakotuadabisha, wakitishiwa, unadhani mradi utaendelea? Si tutabaki na kelele zetu tu?
Ninachotaka, hata tusipige kelele, tuwe tayari kufanya mambo yetu, tuwe na aina fulani ya uwezo wa kutotikiswa mara kwa mara na hawa watu kila wanapotaka kututisha.
 
Nitawakopesha. EU wakae na pesa zao.
 
Asante sana mkuu
 
Mafuta aina yote ya mitambo,lazima ya tumike,mitambo ni vyuma,lazima kuwepo na Oil ya kulainisha hivyo vyuma.Huko viwandani,Oil inatumika kulainishia vyuma visisuguane.
 

Wadau wamaendeleo ya nchi yetu wameanza kukubaliana na msimamo wa nchi uliotolewa na Mh. waziri Mkuu Majaliwa.
Argument kubwa na nzuri ni pamija na matumizi ya petroleum products.
Benki ya Standard imesema hadharani kuwa mradi huu una manufaa makubwa kwa Tanzania na zuganda.
 
Awamu hii wanapenda sana pesa za kudownload.

Wataendelea kupambana na tozo na kuachana na miradi kama hii.
 
Mbona kimafumbo zaidi waogopa nini? Aheri usingandika kabisa!
 
Sababu kubwa ya Ulaya kuupinga huu mradi ni vile Uganda ina uhusiano wa karibu sana na Urusi. Hawa watu wana chuki na kiburi huwezi kuamini. Afrika kukitokea mgogoro siku ya pili wanatuma wajumbe kadhaa eti kusuluhisha kwa amani na kwamba vita haina tija. Walikuwa wanatufanya kama watoto wajinga tusiokuwa na issues za kuhalalisha vita. Wao wakijiona wamekomaa na hawawezi kamwe kupigana tangu vita vya 1945. Sasa kumbe wanaona wao ni binadamu tu kama binadamu wengine na wana mihemuko na chuki zile zile. Inawauma sana hii vita ya Ukrania. Imewaumbua!
 
Wenye uchungu na nchi hii wako wengi tu toka enzi za Mwalimu.
Miaka hii hakuna mkuu. Akina miguru?. Anajifanya mzerondo kutwa na skafu yenye bendera ya taifa. Kapewa nafasi nyeti anavuruga vuruga tu na kujipigia sana. Yupo na mwenzie makatani kapewa nafasi wizara nyeti,umeme unakatika siku nzima. Kipindi cha mwanzo ametupiga fix eti marekebisho. Marekebisho gani kila siku? kipindi cha Magu umeme ilishaanza kuwa historia kukatika
 
Kuwa mzalendo siyo lazima uwe Waziri.
Kuna wazalendo(unsung heroes) wengi tu wanaowapiga lock hao wanaojiitia uzalendo kumbe wana agenda zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…