Bombardier na Boeing zimepaki Wakati Simba SC Wakitumia Kenya Airways na Ethiopia Airways kwenda Nigeria

Bombardier na Boeing zimepaki Wakati Simba SC Wakitumia Kenya Airways na Ethiopia Airways kwenda Nigeria

Nani alikwambia Babra ndio pisi kali kushinda wote Tanzania, unaweza kuwa na hoja ya msingi ila umechanganya na upuuzi.
Kunogesha, ukipinga Barbara Gonzalez siyo pisi kali lete ya kwako , natural hair and skin tulinganishe japo hoja ni ATCL.
aa.jpg
 
Simba Sc klabu " Baba la Baba " likiwa linakwenda cheza mechi za kimataifa huko Nigeria na Plateu FC, inatarajia kuondoka Leo 24-11-2020 11:45 jioni kutokea Mkoa uliotengwa kimaendeleo kwa wivu wa flani [KILIMANJARO] kwa ndege ya KENYA AIRWAYS.

Simba Fc watapita Nairobi na baadae wata-unga mpaka Ethiopia, {kuna mapigano kati ya Serikali ya Abey na wanyonge wa Tigrey] na hapo Ethiopia simba watalala na kuondoke kwenda Aabuja Nigeria siku inayofuata kwa ndege ya ETHIOPIA AIRLINE.

Wakati Tanzania tukijigamba kuwa na ndege inayotoka DAr mpaka Mumbai bila kutua hata kituo kimoja imeshindwaje kuwakodishia simba ndege hiyo waende Nigeria moja kwa moja kupunguza gharama za kuzunguka nchi zaidi ya tatu?

Ukiangalia kwa umakini utagundua ATCL hawana Marketing Managers wala officers, ni waru flani walichomolewa kindugu wakapachikwa hapo lakii hawana strategy yeyote kabisa.

inasemekana Mo-Dewji [Mdosi] alikuwa akiwasilina nao lakini wakadengua na hivyo akaamua kuendelea na maisha yake.

C.EO wa Simba Barbara Gonzalez ambaye pia inasemekana so far ndio "pisi kali kwa Tanzania" alijaribu kuomba ndege kutoka ATCL ikashindikana, siyo kwa msaada, hapana kwa kukodisha.

Nawapongeza wote mliojitahidi kutafuta ATCL na pia maafisa wa ATCL ofisi ku ya Ohio mnakula mshahara na kutembelea magari mazuri lakini hamna mnalofanya, shirika linahitaji overhaul, ninyi mpangiwe kazi nyingine, hata kwenda kufundisha VETA huko Katavi hazina walimu.

Mungu ibariki simba ishinde 2-0.


Kaka kununua Ndege ni tofauti kabisa na kununua gari kwamba ukishakata bima na "fire extinguisher" basi unaingia tu barabarani kwenda popote utakapo. Ndege ni kitu kingine bro!. Kwanza kabisa kabla hujaruhusiwa kutua kwenye viwanja vya wenzetu kuna taratibu nyingi ambazo lazima zipitiwe kufauru vigezo. Kuna maswala ya kuangalia uwezo wa ndege yenyewe, imenunuliwa wapi, uzoefu wa pilotswa nchi na kubwa zaidi na pengine kuhimu kuliko yote ni uzoefu wa shirika lenyewe la ndge kurusha ndege sehemu mbali mbali duniani (Hapo ndio tunakwama).Hata hivyo pamoja na kufauru vigezo vyoote lazima uwekwe kwenye mda wa uangalizi usiopunguwa miaka kadhaa kuangalia uwezo wa shirika lenu la ndege na menginevyo jinsi mtakavyoweza kuingia nchi za watu kwa usalama. Hii ni kutokana na tahadhari kubwa kutokana na aina ya usifiri wenyewe Sasa ni bahati mbaya sisi tulikurupuka kununua ndege mpya bila kufuata ushauri wa wataalam na waliotoa maaumzi aidha kwa kutokuwa na "exposure" au kwa makusudi walikurupuka kununua wakidhani wananunua magari ndio maana dream liner letu linaozea pale airport.
 
Ndege sio daladala kunawatu wamesha weka oda ya kusafiri mwezi mmoja mbaka miwili hauwezi ku acha safari ya Mumbai yenye safari za kudumu tena unauhakika wa abiria 250 ukachukue watu ishirini na kukatisha root.
 
Bombadier haina uwezo wakufly Tz to Lagos ila BOEING 787-8 ambayo inabeba watu zaid ya 200 imebebe watu 20 kwenda Lagos mtalipishwa bei gan?
Ilikuja imebebwa kwenye meli kutoka kwa mabeberu?
 
Wampe tu hata Makonda hiyo kazi ya ku-brand ATCL , kweli sisi ni wa kutumia mandege ya washindani wetu wakati tunazo za kwetu zimepaki na kutu zimeanza?
Tunalaumu bure tu
Msafara Wa Simba ni watu wasiozidi 33 na airbus ni watu 136 hivi....je Simba walikuwa tayari kulipia ndege nzima?

Huwezi ukatoa dege la watu 136 kisa uzalendo wakati running cost ipo pale pale.
 
Ila mtani awali tu kama UD Songo...Wale Plateau biashara yao kuuza wachezaji Ulaya kuna wachezaji wanne kwenye kikosi chao walikuwa waende Ulaya msimu huu Corona ikaharibu deal...kazi mnayo na pira lenu Biriani wanaume wanakula FUFU
 
Hivi yule mtoto wa Prof. Tungaraza bado yupo marketing pale!?
Yule hana uwezo kabisa kabisa.
Yule dada mwenye kichuguu yaani yule dada wa Marketing wa ATCL ni kichwa hasara hana hata akili moja ya kujua nini kifanyike nadhani wameajiri sifa ya kuwa ziada ya mwili wa kukalia.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom