Simba Sc klabu " Baba la Baba " likiwa linakwenda cheza mechi za kimataifa huko Nigeria na Plateu FC, inatarajia kuondoka Leo 24-11-2020 11:45 jioni kutokea Mkoa uliotengwa kimaendeleo kwa wivu wa flani [KILIMANJARO] kwa ndege ya KENYA AIRWAYS.
Simba Fc watapita Nairobi na baadae wata-unga mpaka Ethiopia, {kuna mapigano kati ya Serikali ya Abey na wanyonge wa Tigrey] na hapo Ethiopia simba watalala na kuondoke kwenda Aabuja Nigeria siku inayofuata kwa ndege ya ETHIOPIA AIRLINE.
Wakati Tanzania tukijigamba kuwa na ndege inayotoka DAr mpaka Mumbai bila kutua hata kituo kimoja imeshindwaje kuwakodishia simba ndege hiyo waende Nigeria moja kwa moja kupunguza gharama za kuzunguka nchi zaidi ya tatu?
Ukiangalia kwa umakini utagundua ATCL hawana Marketing Managers wala officers, ni waru flani walichomolewa kindugu wakapachikwa hapo lakii hawana strategy yeyote kabisa.
inasemekana Mo-Dewji [Mdosi] alikuwa akiwasilina nao lakini wakadengua na hivyo akaamua kuendelea na maisha yake.
C.EO wa Simba Barbara Gonzalez ambaye pia inasemekana so far ndio "pisi kali kwa Tanzania" alijaribu kuomba ndege kutoka ATCL ikashindikana, siyo kwa msaada, hapana kwa kukodisha.
Nawapongeza wote mliojitahidi kutafuta ATCL na pia maafisa wa ATCL ofisi ku ya Ohio mnakula mshahara na kutembelea magari mazuri lakini hamna mnalofanya, shirika linahitaji overhaul, ninyi mpangiwe kazi nyingine, hata kwenda kufundisha VETA huko Katavi hazina walimu.
Mungu ibariki simba ishinde 2-0.