Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Nadhani wewe hujui kuwa nchi ni watu waishio pale siyo waliozaliwa pale wenye asili ya pale. Iwapo Einstein alizaliwa Ujerumani lakini akafanyia mambo yake akiwa mmarekani, ni lazima ukubali kuwa huyo ni mmarekani siyo mjerumani tena. Marekani ya asilia ni ya wahindi wekundu, lakini sera zake zinavuia watu wengi kuhamia na kuifanya iwe nchi ya maajabu. Bomu la nyuklia la kwanza lilitengezwa na kutumiwa na wamarekani siyo wajerumani. Ukitaka kutafuta vyanzo vya watu basi hata hao wajeurmani siyo wa huko bali ni wa kutoka Olduvai Gorge hapa Tanzania
Nilikuwa nakusahihisha pale uliposema kwamba Urusi amekopi Marekani kuhusu teknolojia ya kutuma vyombo space na ndiyo nikakwambia kwamba hata Marekani pia amekopi ktk nchi nyingine hiyo teknologia na wala siyo ya kwake, kwamba NASA iliweza tu kuwa na hiyo teknoliojia baada ya kuchukuwa kwa nguvu Wanasayansi na Wahandisi ktk Ujerumani baada ya Vita kuu ya Pili ya Dunia kuisha Wahandisi kama Werner von Braun ndiyo walioiwezesha NASA kuwa jinsi ilivyo leo hii na Urusi vile vile walichukuwa Wanasayansi kama vile Marekani kama mateka baada ya Vita kuisha ktk Ujerumani na ndiyo waliounda SPUTNIK hivyo wote Urusi na Marekani wamekopi /wameipora ktk Ulaya baada ya Vita kuu ya Pili ya Dunia kuisha!
Kuhusu Nuclear technology ni hivyo hivyo Marekani kama Marekani iliweza tu kuunda Bomu la Nyuklia kwa sababu ilichukuwa wanasayansi wengi sana ktk Ulaya na wengi wao kama mateka wa vita na ndiyo walioshiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye uundwaji wa Bomu la Nyuklia!
Ili uweze kuelewa haya mambo unatakiwa kwanza uanze na Historia ya Bomu la nyuklia lilianzaje! Ilianzia na Mwanasayansi Otto Hahn aliyefanya Nuclear fission kwa mara ya kwanza, kila kitu kilianzia hapo...!