PreGE2025 ‘Bon Yai’ Meneja Kampeni wa Freeman Mbowe, ajiunga na Kambi ya Tundu Lissu.. No reforms, no Election

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni uamuzi wake. Kama ambavyo wakina Mrema ni uamuzi wao. Ajabu ni kuwa wakina Mrema mnadai ni waganga njaa wakati huyu mnadai ni mwerevu. Kitu kibaya ni kuwa kutokana na mchezo ulioanzishwa nae atamiminiwa matusi na shutuma kibao. Inasikitisha sana.

Amandla...
 
Haya Mambo yasikie tu. Kwenye maandiko utakutana na UASI WA ABSALOM. tifu lilikuwa Kati ya mtoto na baba mtoto alifanikiwa kukalia kiti cha baba yake Daudi na Daudi hakuwa na jinsi ikabidi asepe kupitia mlango wa nyuma.
Hoja ikawa Hushai alikuwa rafiki ya Daudi Daudi akakataa Hushai kuambatana naye akamwamuru arudi Yerusalem awe informer wa Daudi kificho aliporudi ABSALOM alishangaa sana imekuwaje Hushai kakataa kuambatana na Daudi rafikiye?. Hushai akawa mnyenyekevu kwa Absalom na ABSALOM akamridhia awe kwenye bodi ya ushauri kukata story Hushai alibatilisha maamuzi ya Aisotheferi ambayo kiukweli ndiyo yangemuangamiza Daudi na kuimalisha kiti cha Absalom. Mwishowe Absalom akafia katikati ya mapambano.

Naomba tumuombee sana Lisu akifanikiwa Tanzania imepona dhidi ya akina Hushai.
 
Tuwe makini na huyu jamaa
 
Kwamba G55 ni bumbumbu kiasi cha kuelimishwa na Mwenyekiti wa sasa?! Hivi uasi unapewaje Elimu?! Dawa ya uasi haijwahi kuwa Elimu.
 
Si Mwana CDM tubali tunasema mtanganyika yoyote mwenye akili timamu lni azima asonge mbele na Lissu.

Lissu hakuuawa siku ile maana mpango wa Mungu ulikuwa haujakamilika wa kurutoa mikononi mwa wakoloni CCM.

Tunaomba msamaha sisi tuliokubeza wakati wa uchaguzi wa ndani.

No reform...no election - wewe ni mtu sahihi kuivusha tanganyika kuelekea mageuzi ya kweli.
 
Asije kuwa katumwa kimkakati kama yule kijana Malya aliyeishi na Chacha Wangwe 2007 pale Dodoma. Duuh. Hivi kumbe nimetoboa sehemu ya Siri.
 
Bado kigogo wa kanda ya Nyasa haijulikani yupo na Lissu au genge la G55
 
Kwamba G55 ni bumbumbu kiasi cha kuelimishwa na Mwenyekiti wa sasa?! Hivi uasi unapewaje Elimu?! Dawa ya uasi haijwahi kuwa Elimu.
Kwa akili zangu za kiaduje, mtu mkorofi saa nyingine nenda naye hatua hatua ili kuweka kumbukumbu sawia kwenye jamii ya watanzania mwisho wa siku hata watu wa kijijini watajua kuwa yupi ambaye yupo upande wa maslahi ya taifa au yupi upande wa maslahi ya wenye mamlaka
 
Bon chama kinakuhitaji katika mapambano achana na kundi la Mbowe watakupotezea uaminifu kwa makamanda katikati ya Vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…