Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Penologist

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
790
Reaction score
1,923
Salaaam wakuu,

Nimekuwa nikisikiliza mziki wa bongo flava kuanzia enzi za takeu ikaja kiduku, ikaja ngololo hadi kufikia mpelekee moto.

Ukweli ni kwamba hapo nyuma walianza vizuri kwa upande wa hiphop kina niger j na Mr.2 wakatengeneza njia wakaandika mashairi ya kuelimisha jamii na wengine waka fanya hiphop cartoon ambayo inaelimisha na kuburudisha. Watu tukaelewa mziki wa bongo tukasikiliza hadi sitting room tukiwa familia nzima.

Kwa upande wa bongo flava tulisikiliza tungo nzuri za mapenzi kina T.I.D,Matonya,Mb doggy na Mr.Nice waliandika nyimbo za mapenzi zenye staha unazoweza sikiliza na familia watu tukauelewa mziki wa bongo.
Wakaendelea vizuri ukaja mziki wa kucheza wenye tungo hafifu lakini hakuna matusi, tuta wakumbuka kina msami, mesen selecta, diamond wa number one, Ali wa chekecha, shetta wa kerewa na wengine.

Miaka ya hivi karibuni sasa ndiyo imekuwa tatizo mziki ni matusi na ngono mubashara tungo zimekuwa explicit yaani unaogopa hata kusikiliza ukiwa pekeyako licha ya kuwa na familia, mziki uliotawaliwa na tungo za ngono tupu, mziki usiokuwa na staha, kila upande ni vurugu siyo hiphop wala bongo flava, maneno utakayo sikia ni mpelekee moto huyo ni baddest, yupo young lunya atakuambia habari za kupeleka moto hadi kukojoza mara mpe tango,lulu diva ata kuambia anapenda Mandingo ina mkolea kitandani utasikia napenda inavyo zama. Tpuu naona aibu ata kuandika hapa.

Mziki wa bongo flava umekuwa kielelezo cha maadili kuporomoka kwa kiwango cha sgr. Rai yangu kwa basata fungieni huo uozo ata kama zikitoka nyimbo chache zenye heshima ni bora mpaka pale wasanii watakapo jifunza kuandika tungo zenye maadili.
 
Salaaam wakuu,
Nimekuwa nikisikiliza mziki wa bongo flava kuanzia enzi za takeu ikaja kiduku, ikaja ngololo hadi kufikia mpelekee moto.

Ukweli ni kwamba hapo nyuma walianza vizuri kwa upande wa hiphop kina niger j na Mr.2 wakatengeneza njia wakaandika mashairi ya kuelimisha jamii na wengine waka fanya hiphop cartoon ambayo inaelimisha na kuburudisha. Watu tukaelewa mziki wa bongo tukasikiliza hadi sitting room tukiwa familia nzima.

Kwa upande wa bongo flava tulisikiliza tungo nzri za mapenzi kina T.I.D,Matonya,Mb doggy na Mr.Nice waliandika nyimbo za mapenzi zenye staha unazoweza sikiliza na familia watu tukauelewa mziki wa bongo.
Wakaendelea vizuri ukaja mziki wa kucheza wenye tungo hafifu lakini hakuna matusi, tuta wakumbuka kina msami, mesen selecta, diamond wa number one, Ali wa chekecha, shetta wa kerewa na wengine.

Miaka ya hivi karibuni sasa ndiyo imekuwa tatizo mziki ni matusi na ngono mubashara tungo zimekuwa explicit yaani unaogopa hata kusikiliza ukiwa pekeyako licha ya kuwa na familia, mziki uliotawaliwa na tungo za ngono tupu, mziki usiokuwa na staha, kila upande ni vurugu siyo hiphop wala bongo flava, maneno utakayo sikia ni mpelekee moto Hugo ni baddest, yupo young lunya atakuambia habari za kupeleka moto hadi kukojoza mara mpe tango,lulu diva ata kuambia anapenda Mandingo ina mkolea kitandani utasikia napenda inavyo zama. Tpuu naona aibu ata kuandika hapa.

Mziki wa bongo flava umekuwa kielelezo cha maadili kuporomoka kwa kiwango cha sgr. Rai yangu kwa basata fungieni huo uozo ata kama zikitoka nyimbo chache zenye heshima ni bora mpaka pale wasanii watakapo jifunza kuandika tungo zenye maadili.
We mpelekee moto ,mpelekee moto..!
 
Ila ndo wanapiga hela kuliko hao wa zamani na ndo kitu cha muhimu.

Zama zina badilika, na binaadam pia hubadilika huenda hizi ndo zama za matusi n.k
 
Mkuu mzee ni nani?, ninavyojua wazee mziki wao ni rhumba za taratibu za akina mbaraka na marijani.
Mzee n wewe unaetaka nyimbo za aina yako, tuache bhana watoto tuburudike na miziki ya matusi wakati wetu huu.
 
Pesa imekuwa kisingizio cha kuimba ngono, Mr.Nice alijaza ela ya matumizi kwenye boot ya gari na hakuimba matusi.
Ilikuwa zama hizo mkuu, ndo maana nikasema zama zimebadilika sasa hivi usipoimba matusi mambo hayaendi.

Sipendi matusi na ni mdau mkubwa wa ngoma za kitambo.

Angalia hata hip-hop za siku hizi wanaimba vitu havieleweki muhimu vina, yaani unasikiliza wimbo hakuna logical sequence hujiui nini hasa kinazungumzwa.

Ila ukirudi nyuma enzi za kina professor J, enzi hizo anajiita nigger J, au kina afande na two proud au Mr two kuna tofauti kubwa sana.

Ila ndo hivyo zama zimebadilika
 
"Weka mate niteleze, kama nyoka pangoni.."
"Nalegea, ikigusana yangu na yakoo.."
"Sitaki kibamia, mwanaume mashine.."
"Kutwa nadindisha mkonga.."
"Mtoto laini, chuchu dodo dodo.."
Naona aibu Mimi.
 
Usioonee Bongo fleva tu, muziki wa kisasa hata huko Marekani ndio wanavyoimba hivyo. Unamsikiliza tu Chris Brown lakini maneno ya kwenye nyimbo zake huyaelewi. Au umeshawahi kusikiliza WAP ya Cardi B?
Nicki Minaj aliwahi kuulizwa anajisikiaje nyimbo zake zikisikilizwa na watoto? Akajibu kwa ufupi tu, akasema, mimi sio mama yao.
Kwa kifupi endelea kumsikiliza Rose Muhando tu, haya mambo mengine waachie wengine. Period.
 
Back
Top Bottom