Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa hivi mziki ni matusi ila zamani sio matusi yani umeweka double standard kwanini??Nope sijamaanisha wote,wapo wachache wanafanya vizuri.Kama unabisha washa radio au television ukiwa na mtu unaye mheshimu 3/4 ya nyimbo zitakazo chezwa ni ngono tupu.
Kiukweli hata Mimi sisikilizi nyimbo hzo aisee , japo wapo wanaozipenda Ila hamna kitu ....mara moja moja wanajaribu, rayvanny nyimbo zake za slow waweza sikiliza Ila hzo nyegezi mhhhh
Ndiyo mziki wa sasa ni ngono tupu corus na verse zote ni matusi jirekebisheni wasanii.sasa hivi mziki ni matusi ila zamani sio matusi yani umeweka double standard kwanini??
Dully Sykes anakuambia "nipe japo kiduchu nishachoka kupiga puchu"
KR Mulla anakuambia "we ukitaka tende chukua lakini .... unapanua"
unataka za Temba??
Hata zamani matusi yalikuwepo bwana tena ya wazi tu ila walichobarikiwa ni kwamba mashairi yao mpaka bado yanaishi tofauti na sasa.
Salaaam wakuu,
Nimekuwa nikisikiliza mziki wa bongo flava kuanzia enzi za takeu ikaja kiduku, ikaja ngololo hadi kufikia mpelekee moto.
Ukweli ni kwamba hapo nyuma walianza vizuri kwa upande wa hiphop kina niger j na Mr.2 wakatengeneza njia wakaandika mashairi ya kuelimisha jamii na wengine waka fanya hiphop cartoon ambayo inaelimisha na kuburudisha. Watu tukaelewa mziki wa bongo tukasikiliza hadi sitting room tukiwa familia nzima.
Kwa upande wa bongo flava tulisikiliza tungo nzri za mapenzi kina T.I.D,Matonya,Mb doggy na Mr.Nice waliandika nyimbo za mapenzi zenye staha unazoweza sikiliza na familia watu tukauelewa mziki wa bongo.
Wakaendelea vizuri ukaja mziki wa kucheza wenye tungo hafifu lakini hakuna matusi, tuta wakumbuka kina msami, mesen selecta, diamond wa number one, Ali wa chekecha, shetta wa kerewa na wengine.
Miaka ya hivi karibuni sasa ndiyo imekuwa tatizo mziki ni matusi na ngono mubashara tungo zimekuwa explicit yaani unaogopa hata kusikiliza ukiwa pekeyako licha ya kuwa na familia, mziki uliotawaliwa na tungo za ngono tupu, mziki usiokuwa na staha, kila upande ni vurugu siyo hiphop wala bongo flava, maneno utakayo sikia ni mpelekee moto Hugo ni baddest, yupo young lunya atakuambia habari za kupeleka moto hadi kukojoza mara mpe tango,lulu diva ata kuambia anapenda Mandingo ina mkolea kitandani utasikia napenda inavyo zama. Tpuu naona aibu ata kuandika hapa.
Mziki wa bongo flava umekuwa kielelezo cha maadili kuporomoka kwa kiwango cha sgr. Rai yangu kwa basata fungieni huo uozo ata kama zikitoka nyimbo chache zenye heshima ni bora mpaka pale wasanii watakapo jifunza kuandika tungo zenye maadili.
Siyo kila kitu cha kuiga mkuu, Rashidi benzino awe Omar shakur kweli,waige na kupigana risasi basi.2pac alishawahi kusema kuwa., sisi ni ma'rapa, tunaimba vitu tunavyoviona na kuvifanya, tukiimba kuwa tunavuta bangi, ni kweli tunavuta bangi, kwa hiyo wazazi inabidi wafanye kazi yao.
Kwa hiyo acha kulalamika mzee.
Mkuu nakubaliana....ila wa sasa wanaenda na soko linavyotaka....na ndo wamepaisha fani kimataifa...Salaaam wakuu,
Nimekuwa nikisikiliza mziki wa bongo flava kuanzia enzi za takeu ikaja kiduku, ikaja ngololo hadi kufikia mpelekee moto.
Ukweli ni kwamba hapo nyuma walianza vizuri kwa upande wa hiphop kina niger j na Mr.2 wakatengeneza njia wakaandika mashairi ya kuelimisha jamii na wengine waka fanya hiphop cartoon ambayo inaelimisha na kuburudisha. Watu tukaelewa mziki wa bongo tukasikiliza hadi sitting room tukiwa familia nzima.
Kwa upande wa bongo flava tulisikiliza tungo nzri za mapenzi kina T.I.D,Matonya,Mb doggy na Mr.Nice waliandika nyimbo za mapenzi zenye staha unazoweza sikiliza na familia watu tukauelewa mziki wa bongo.
Wakaendelea vizuri ukaja mziki wa kucheza wenye tungo hafifu lakini hakuna matusi, tuta wakumbuka kina msami, mesen selecta, diamond wa number one, Ali wa chekecha, shetta wa kerewa na wengine.
Miaka ya hivi karibuni sasa ndiyo imekuwa tatizo mziki ni matusi na ngono mubashara tungo zimekuwa explicit yaani unaogopa hata kusikiliza ukiwa pekeyako licha ya kuwa na familia, mziki uliotawaliwa na tungo za ngono tupu, mziki usiokuwa na staha, kila upande ni vurugu siyo hiphop wala bongo flava, maneno utakayo sikia ni mpelekee moto Hugo ni baddest, yupo young lunya atakuambia habari za kupeleka moto hadi kukojoza mara mpe tango,lulu diva ata kuambia anapenda Mandingo ina mkolea kitandani utasikia napenda inavyo zama. Tpuu naona aibu ata kuandika hapa.
Mziki wa bongo flava umekuwa kielelezo cha maadili kuporomoka kwa kiwango cha sgr. Rai yangu kwa basata fungieni huo uozo ata kama zikitoka nyimbo chache zenye heshima ni bora mpaka pale wasanii watakapo jifunza kuandika tungo zenye maadili.
Ila matusi yamezidi...Mziki wa matusi ni haki yako ya msingi?.
Kuna vitu vikifika level fulani ni ngumu kuvizuia bali kuvitengenezea mazingira na utaratibu mzuri.Siyo kila kitu cha kuiga mkuu, Rashidi benzino awe Omar shakur kweli,waige na kupigana risasi basi.
Muda wa kuimba matusi sio?Muda wao huu
Wamekosa vya kuimba, sasa ni ujinga mtupu na matusiKuna wimbo mpya Unaitwa NIMETOA KITU maanake kaachia ushuzi kujamba nmecheka sana.
Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Basata na Tcra wafanye hili kuokoa kizaziKuna vitu vikifika level fulani ni ngumu kuvizuia bali kuvitengenezea mazingira na utaratibu mzuri.
Kuna kipindi niliwahi andika uzi humu wa kufanya censorship ya nyimbo kwa utaratibu huu.
1. Mamlaka zinazohusika na kusimamia sanaa ziandae mgawanyo wa kimaudhui. Mfano nyimbo zote zinazotaja mambo ya ngono, vilevi, madawa ya kulevya, matumizi ya silaha ziwekwe kwenye kundi tuliite labda E'rated. Halafu nyingine zenye maudhui ya kawaida ziwe rated kama tuseme labda A'rated. Na mwongozo huu unatakiwa ufuatwe na kila msanii.
2. Msanii anapotaka kutoa wimbo lazima aufanyie tathmini ili ajue unadondokea wapi kati ya E'rated au A'rated na atatakiwa au'lebel kulingana na kundi unapodondokea.
3. Nyimbo zote ambazo ni E'rated hazitatakiwa kuchezwa redioni, kwenye tv, kwenye saluni au eneo lolote la umma. Na yeyote ambaye atabainika itabidi aadhibiwe kulingana na sheria ambayo itakuwa imetungwa (inatakiwa iwe kali sana). Nyimbo ambazo ni E'rated zitapatikana mitandaoni tu sehemu ambapo mtu anainngia kwa ridhaa yake.
4. Kama msanii ana wimbo ambao ni E'rated na anataka uchezwe redioni au kwenye tv, basi anapaswa kutengeneza clean version ambayo itakuwa rated kama A'rated.
Huu ni utaratibu mzuri unaohitajika kwa sasa ila unahitaji usimamizi wa karibu sana ili ufanye kazi. Bora huku kuliko kupiga kelele nyimbo zifungiwe kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wa filamu wanafanya hii kitu, tofauti ni kuwa kwa wao ni lazima upeleke filamu yako wanaikagua then wanaipa daraja.