Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

sasa hivi mziki ni matusi ila zamani sio matusi yani umeweka double standard kwanini??

Dully Sykes anakuambia "nipe japo kiduchu nishachoka kupiga puchu"

KR Mulla anakuambia "we ukitaka tende chukua lakini .... unapanua"

unataka za Temba??

Hata zamani matusi yalikuwepo bwana tena ya wazi tu ila walichobarikiwa ni kwamba mashairi yao mpaka bado yanaishi tofauti na sasa.
Lugha yao ilikuwa na staha sana..

Walitumia sanaa yao vizuri..

Sio hawa wa sasahivi wanachana waziwazi..

😀😀😀
 
Kama utakuwa unafikiri vizuri,utaona tofauti kati ya wimbo wa matusi na wimbo wa mapenzi.

Siwalaumu sana wasanii wa sasa kwa vile wengi IQ yao ni ndogo.Badala ya kuimba nyimbo za mapenzi kama walizoimba wanamuziki wa zamani,mfano Marijani,na wengine wengi,wao wanaimba matusi live.Sijui nataka muhogo,ingiza yote,sijui nasikia utamu nikimumunya..na ujinga kama huo.

Ninachoona kwa wengine kama sisi,inanisaidia sana kuishi kwa utulivu masaa mengi kwa vile sifungui Redio na nikuwasha TV kama ni lazima ninai mute tu na kusibiria taarifa ya habari ama vipindi vya kuelimisha.

Nyie endeleeni tu sie wengine tulishaacha kusikiliza
Shida JF wengi ni watu wazima na Familia zao. Ila mimi kama msanii siwezi kuacha kutunga wimbo kisa eti kuna watoto. Watoto Wana wazazi na walezi kazi yao ni Nini? Arguments zenu nyingi it's about "watoto watajifunza nini? Hawa wasanii SIO BABYSITTERS hawako kwa ajili ya kukulelea wewe mtoto wako.

Mbona hamsemi pombe zifutwe, kwani watoto hawaoni hizo pombe? Mtoto wako akiwa mlevi utailaumu TBL au wewe mzazi mwenyewe ndo inabidi ulaumiwe?

Huo muziki wa kuelimisha vitu km ukimwi n.k ni wa kipindi hicho ambapo Watanzania wengi walikuwa hawana elimu. Ila kwenye hii nchi ambayo hata mtoto wa darasa La Tatu anafundishwa kuhusiana na Ukimwi, kweli Kuna ulazima wa wasanii kuimba nyimbo kama hizo? Kuna mtu asiyejua ukimwi Unaua? Au nyimbo sijui kuhusiana na ndoa, kweli? Kwenye age hii ambayo everything is found on the internet yaani?

As a country going to a middle class phase muziki na entertainment vinafanya kazi moja tu. Kuburudisha. That's it. Hayo mambo ya kuelimisha sijui kutoa elimu kwa jamii sio jukumu La wasanii. Shule zina kazi gani sasa?

Alafu mbona juzi juzi tu hapa Rayvanny alitoa wimbo wa "kuelimisha" kuhusu Corona? Hamkuskia?
 
Kama utakuwa unafikiri vizuri,utaona tofauti kati ya wimbo wa matusi na wimbo wa mapenzi.

Siwalaumu sana wasanii wa sasa kwa vile wengi IQ yao ni ndogo.Badala ya kuimba nyimbo za mapenzi kama walizoimba wanamuziki wa zamani,mfano Marijani,na wengine wengi,wao wanaimba matusi live.Sijui nataka muhogo,ingiza yote,sijui nasikia utamu nikimumunya..na ujinga kama huo.

Ninachoona kwa wengine kama sisi,inanisaidia sana kuishi kwa utulivu masaa mengi kwa vile sifungui Redio na nikuwasha TV kama ni lazima ninai mute tu na kusibiria taarifa ya habari ama vipindi vya kuelimisha.

Nyie endeleeni tu sie wengine tulishaacha kusikiliza

Wewe kuangalia taarifa ya habari does not mean you are intelligent than the rest.

Kila mtu atakula alikopeleka mboga.
 
Back
Top Bottom