Sambinyakwe kitololo
JF-Expert Member
- Nov 15, 2022
- 2,419
- 2,940
Nimeenda duka la simu kuulizia kitu fulani, mwenye duka alishakuwa maarufu ndiyo maana niliagiziwa pale, nimeshangaa sana yuko makini na Instagram, hanisikilizi. Mara ana 'screenshot' Instagram anamtumia mfanyakazi wake namuongelesha hanisikilizi.
Hivi tutafika kweli kwa mtindo huu? Kwamba duka kujaa vitu anadharau elfu 30 yangu. Hivi Wabongo kuwa na ka duka ka spea za simu, simu mpya/zilizotumika, chaja n.k unaona kama Dunia yote yako? Dah! Imeniuma sana.
Hivi matajiri wenzetu huko mambele na wenyewe wanadharau? Ile kukudharau sababu unanunua labda 'earphone' za elfu 5, hajui pesa ndogo na kubwa ndiyo zimemfanya afikie hapo kwa sasa.