Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Sijajua mikoa mingine ila kwa michache niliyotembelea naona ni hizi series za kikorea zilizotafsiliwa. Na wengine ndo izo movies na series za nje, nyuzi zilizopo humu kuhusu masuala ya filamu pendwa zinathibitisha hilo. Hawajadili movie za bongo ni za nje tu.
Mimi nilivyoanza kushuhudia jinsi wanavyoandaa na kuona uongo wanaotumia hapohapo nilianza kuzipotezea yaani nilianza kuona jinsi wavyompaka tomato kisingizio kama damu
 
Ndio hivo mkuu sometimes huo ni kama utani kazini aisee.
Nilishuhudia film nyingi sana zikishutiwa nyingine hadi kwenye mageto yetu mtu anakuomba naomba nishoot kwenye chumba chako pia nilishawahi kuwashikia mpaka boom la kuchukua sauti yaani nikawa nipo jikoni nashuhudia uongo woote
 
Nilishuhudia film nyingi sana zikishutiwa nyingine hadi kwenye mageto yetu mtu anakuomba naomba nishoot kwenye chumba chako pia nilishawahi kuwashikia mpaka boom la kuchukua sauti yaani nikawa nipo jikoni nashuhudia uongo woote

Mkuu kuna makweli kwenye filamu? hata huko majuu pia ni uongo tu, au unafikiri zile risasi wakipigana hua ni za kweli na damu za kweli?
 
Bongo movie INA safari ndefu sana maana.mm naamin wakiwa serious na wakafanya kazi nzur wawekezaji watakuja weng na wakutosha,nenda kaangalie wasouth na wanaija huko Netflix.
Kuna series mmoja huko Netflix y kisauzi jina lake sikumbuki ila inahusu msichna mmoja anaenda shule ya matajiri kumtafuta pacha wake,ni series ya kawaida hata aina budget kubwa ila n nzuri

Blood & water ..... bongo movie kufikia level zile labda magufuli afufuke
 
Pia kuna kampuni ilikuwepo ilikua inaitwa Wananchi video productions store ambayo ilikuwa inasambaza film za Jumanne kihangala na Mussa Banzi nayo ilisitisha usambazaji kipindi cha kikwete na 7bu ilikua ni uigizaji mmbovu wa wasanii

Film za Mussa zilikua kiboko
 
Mimi bado nakupinga mkuu ni vile tu hatujajizatiti huko naungana na mtoa uzi 100%. Tasnia imejaa wasioelimika kuhusu hiyo kazi yao. Japo uchumi ni changamoto lakini unaona kabisa jinsi hata hiyo pesa kidogo wanavotumia kutuonesha madudu kwenye filamu zao nyingi zenye story moja yenye kisa kinachofanana (MAPENZI).

Wasanii wa muziki miaka ya zamani hawakua watu wa kwenda kushoot video zao nje na kushirikisha saana wasanii toka nje ya nchi. Lakini hivi karibuni baada ya kuona wenzao wanaenda sana kushoot nje na wanashirikisha wasanii wakubwa wa nje nao wameiga icho kitu na kinawapa matokeo chanya. Ona jinsi tasnia ya muziki inavopaa, mfano ni hawa wasanii kina maroo,mboso na wanaofanana na hao.

Haya tuje kwenye filamu zamani ilikua inafanya poa sana na iliteka sana soko la bongo ikichuana na nigeria, hizi za kikorea zimekuja hivi karibuni tu labda za kihindi na kizungu ndio zilitamba sana enzi hizo nazo ilikua ni vibanda umiza majumbani ilikua bongo movies. Akaja kanumba nae akaipaisha mno, Ray nae hakua nyuma. Je hawa wasanii waliobaki walicopy nini toka kipindi kile sanaa iko juu, enzi za kanumba & Ray, yaan hakuna la kujifunza kabisa kwa hivyo vyote kama wenzao wa muziki wanavyonata na soko lao.
Huyu Ray alikuwa mtembelea nyota ya Kanumba tu kupitia haters wa Kanumba. Kanumba aliiamsha bongo movie kwa ubunifu wake mkubwa na kujaribu mambo mapya( jamaa alienda hadi Nigeria kushoot Movie). Hakukuwa na bado hatujapata msanii anaemfikia Kanumba kwenye ubunifu wengi wao kipindi kile walikuwa wababaishaji ila upepo wa mafanikio ya Kanumba uliwapitia na wao.
 
Film za Mussa zilikua kiboko
Kabisa mkuu, yaani jamaa serikali ingemsapoti angekua mbali sana
Ila p1 na movie zote alizoandaa kuna siku nilikutana naye anatembea kwa miguu hana hata baiskel
 
Mtoa mada kaandika vizuri, ila baada ya muda wadau wanatia matusi,vitisho,masimango na vitu vingine vya hovyo.

Haujengi kwa kutukana, ukitaka mabadiliko wewe uwe wa kwanza kubadilika.
 
Umeongea vizuri..chuo cha sanaa Bagamoyo kinao na kinatoa wataalamu. Naunga mkono hoja ya faza nelly ya ukosefu wa mitaji.
Angalia sinema zile za miradi mfano malaria au uzazi ambazo zinakuwa na ufadhili mzuri zinakuwa bora kwa kuwatumia waigizaji wale wale lakini wanakuwa kwenye uangalizi na waongozaji waliosomea. Ukitaka kuthibitisha hili angalia sinema ya CHUMO.
Kweli Mkuu CHUMO haichoshi angalia pia Siri ya mtungi na Hukumu ya tunu .
 
  • Thanks
Reactions: BRN
BONGO MOVIE WENGI NI VILAZA, SIO AJABU WAMEILAZA SANAA YA UIGIZAJI.

Anaandika, Robert Heriel.

Hapana shaka sanaa ya Uigizaji kwa sasa imelala Usingizi wa Pono, imelala fofofo na waigizaji wake wanakoroma. Wapo kwenye ndoto za majinamizi wabaya wanaowakimbiza kwenye mitaro huko usingizini. Tangu kifo cha Marehemu Kanumba miaka zaidi ya tisa iliyopita Tasnia ya Bongo Movie imelala fofofo.

Hakuna Tasnia inayoongozwa na Vilaza isilale, sijawahi kuona popote pale duniani. Bongo Movie imejaa wasanii vilaza kwa kiwango kikubwa sana, watu waliokimbia shule ndio wamekimbilia huko kwenye tasnia ya filamu. Embu fikiria mtu amekimbia shule kwa kushindwa somo hata la kiswahili unafikiri atatuambia nini kwenye suala la kuelimisha jamii kupitia fani ya uigizaji.

Kilaza ni kilaza tuu, uwezo wake wa kufikiri ni mdogo alafu anakuwa Director wa filamu, unafikiri filamu yake itakuwaje kama sio Utopolo. Kilaza hufikiri mambo chini ya kiwango, ukiwaangalia wasanii wengi wa bongo movie wakiigiza kwanza hawawezi kuuvaa uhusika, wanachojua ni kutoa macho, kukenua, kubinua makalio, kuvaa nguo fupi, wakati kwa upande wa wasanii wa kiume wanachjua ni kupaka piko sijui waves nywele zao, kutoboa masikio au kubandika stiker masikioni, na kulamba lamba midomo kama sio kusuka nywele. Kwa mambo haya wamefuzu kwani mambo haya hufanywa kwa sehemu kubwa na vilaza, kwani hata mtu asiye msanii anaweza kufanya mambo hayo. Vilaza hufanya mambo ambayo mtu yeyote anaweza kufanya.

i/ Muongoza Filamu alifeli shule, akaunga unga wee akapata cheti, huyo akajiingiza kwenye Tasnia ya Filamu, haya embu niambie atatupa kipi cha maana hapo?
ii/ Mtayarishaji alifeli shule, akaunga unga wee, embu niambie ataleta jambo gani katika ulimwengu huu wa elimu, sayansi na teknolojia?
iii/Mchukua Kamera alipata sifuri au four ya mwisho kabisa, hivi unategemea atakuwa na ubunifu gani kwenye masuala ya kurekodi picha na video na kamera?
iv/ Mtia sauti, aliishia kidato cha nne, embu niambie anauelewa gani na mambo ya sauti, muziki na ala? Sio ajabu sauti nyingi zinazoingizwa kwenye movies nyingi ni zile zile haziendani na uhalisia,
v/ Mtu wa Makeup aliishia darasa la pili, hivi anajua nini kuhusu urembo? Kama utabisha angalia filamu zetu kisha angalia za wenzetu kama wanaijeria utaelewa.
vi/ Mtu wa simulizi, aliishia darasa la saba, hivi unafikiri uwezo wake wa kufikiri, na uelewa wa mambo ataandika script ipi yenye kufanya kizazi cha sasa kukubali kisa chake

Shida kubwa ya Wasanii wa Bongo Movie ni elimu ni ndogo sana kwa wengi wao, wengi ni Slow Learner, wachache sana wanauwezo mkubwa wa kiakili, kufikiri na kuchambua mambo. Wengi wao ni bora liende nao wawemo.

Ukitaka kujua kuwa Wasanii wetu wengi wao ni Vilaza basi angalia Role Model wao waliopo ughaibuni kama Marekani, bado ni wale wale waliokimbia shule, watu wenye Skendo, wavaa uchi, watumiaji wa madawa ya kulevya, na wahuni walioshindikana.

Bongo Movie ikataka iinuke iache kuchukua Vilaza, slow Learner watu waliokimbia shule ambao kimsingi lazima wawe na akili finyu na kazi zao lazima ziwe duni.

Waigizaji wengi wa Nigeria, Ghana, South Afrika wana elimu Degree moja kuendelea, yaani ambao hawajasoma ni wachache sana ukilinganisha na wenye shahada. Ndio maana wanajua kile wafanyacho. Embu angalia filamu na tamthilia za Kikorea ambazo kwa sasa zinateka soko hapa nchini, waigizaji karibu wote wa Kikorea ni Wasomi wa elimu ya juu kabisa kuanzia Degree tena nyingine ni zile za moto. Njoo kwa Wahindi, wafilipino, na kule Amerika ya kusini, waigizaji karibu wote ni wasome wa elimu ya juu kabisa.

Mtu mwenye elimu ya uhakika sio ile elimu ya kuunga unga kwenye vyuo visivyoeleweka hawezi kutoa kazi mbovu.

Naipongeza serikali kwa kuanzisha michepuo mipya itakayoendana na mambo ya sanaa na Lugha ili kufufua Tasnia ya Filamu hapa nchini.

Mtu kaishia Darasa la saba au kidato cha nne, atajuaje na kuigizaje mambo ya Ujasusi wa kidola na kiuchumi yaani ataanzia wapi?
Mtu madarasa hayamtoshi, ataweza kuigiza filamu za kisiasa, ugaidi, na masuala ya demokrasia? Atawezaje ikiwa hajui hata historia ya hiyo demokrasia yenyewe zaidi ya maneno ya mtaani na vijiweni.
Mtu kaishia kidato cha nne atawezaje kufikiria kuandaa scripts ya mambo ya Mpango wa dunia wa milleniam, atawezaje kuigiza Umuhimu wa vyama vingi vya siasa ndani ya nchi?
Mtu kaishia kidato cha nne kwa kulazimishwa, atawezaje kuigiza filamu ya masuala ya sheria na haki za binadamu, hajui hata katiba ya nchi yake, mtu kama huyo huoni ni jipu?

Mtu kaishia kidato cha nne, atawezaje kuandaa filamu ya athari ya udikteta na ukosefu wa uhuru wa kujieleza ndani ya jamii,lini atawaza hayo, yeye kama sio kuwaza mapenzi tuu muda wote?

Mtu kaishia darasa la saba au kidato cha nne, atawezaje kufikiri hata kuigiza filamu inayopromoti utalii wa nchi yetu, utashangaa licha ya nchi yetu kuwa na Mbuga na vivutio vingi lakini tangu tupate uhuru hakuna filamu ya wanyama iliyochezwa na wabongo, utashangaa. Ndio shida ya vilaza hiyo. Wenyewe watakuambia uchumi mgumu.

Mtu anaelimu ya kuunga unga, atawezaje kuigiza inayozungumzia masuala ya fani za kitaalamu kama vile Ualimu wenyewe sio ule wa kuigiza kama wanaoigiza watoto kibaba baba na kimama mama. Au udaktari, au sheria, au injinia, utawezaje igiza kitu hukijui na huna akili ya ku-master kwa upesi.

Mimi nawashauri wenye nafasi na wanaotaka Bongo Movie iamke basi wafanye haya;
Wasajili watu wenye vipaji Fresh from the School, waende shule zenye vipaji huko, Vyuo vikuu vinavyotambulika wachukue watu huko.
Wasaniii wawekewe sheria kuwa ili uwe mwigizaji basi yakubidi uwe na elimu isiyochini ya Diploma. Na uwe umefaulu vizuri kidato cha nne

Tasnia inapoongozwa na Kilaza kamwe haiwezi kuzaa matunda chanya kwenye jamii.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Sumbawanga
Excellent
 
Ila tuache masihara hata yule director wa Dhamira aliuwa Sana kwani alibase pande zote yaani siasa,uchumi na mapenzi pia ufisadi ni series moja imetulia sana
 
Back
Top Bottom