Bongo Star Search Wapewa mwezi mmoja kumlipa mshindi wa BSS 2019

Sasa atalipaje na Mengi alishafariki!?
Serikali ingejionheza tu kuwa hawa wanawake wanaojifanyaga wamefanikiwa huwa kuna wanaume wanaosimamia mafanikio yao!!
Mie huwa nashangaa sana hata wale wanaojiita
Malikia wa nguvu kumbe nguvu nyingi huwa ziko viunoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii pesa alitakiwa aitoe MENGI sema ndo vilee mzee ashafariki mambo yamekuwa magumu sanaa.. Hapo ndo utajua nyuma ya kila mwanamke kuna mwanaume aisee[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama Bongo Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019 zawadi yake ya milion 50. View attachment 1412584

==========

Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kuanzia Aprili 08, 2020 kwa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya Bongo Star Search chini ya Mkurugenzi wake Madam Ritha Paulsen kumlipa kiasi cha Shilingi milioni 50 mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa mwaka 2019, Bw.Meshack Fukuta.

Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo leo Jijini Dodoma baada ya kupokea barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa mkononi ambapo Mhe. Naibu Waziri amesisitiza makubaliano yote yalioanishwa kufanyiwa kazi.

“Mimi kama mlezi wa tasnia ya Sanaa ambaye pia nilikua mgeni rasmi siku ya fainali nimesikitishwa sana na malalamiko haya, hivyo naitaka kampuni ya Benchmark kutekeleza ahadi hiyo na wasipofanya hivyo ndani ya muda huo, Serikali haitasita kufungia mashindano hayo”, alisema Mhe.Shonza.

Mhe. Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Benchmark kuhusu malalamiko hayo mbapo Kampuni hiyo ilieleza kuwa imeshindwa kumlipa msanii huyo kutokana na viongozi wa Kampuni iliyodhamini shindano hilo ya Startimes kuwepo nchini China na kushindwa kusafiri kuja nchini kutokana na uwepo wa ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo Mhe.Naibu Waziri ameleeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Startimes ambao umekiri kuwa umeshalipa fedha kwa Kampuni ya Benchmark tangu mwezi Januari 2020.

Aidha, Mhe.Shonza ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inamtengenezea msanii huyo wimbo bora pamoja na kuufanyia matangazo ya kutosha katika kipindi cha miezi miwili kuanzia leo pamoja na kuwasilisha nakala ya mkataba wa washiriki waliofikia hatua ya kumi bora ndani ya wiki moja kuanzia leo machi 08,2020.

Katia hatua nyingine Mhe.Shonza ameliagiza Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA) kusimamia utaratibu wa uaandaji wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa mikataba kati ya wasanii na wanaondesha mashindano au shughuli yoyote ya sanaa na wasanii pamoja na kuhakikisha ahadi wanazopewa washindi ikiwemo zawadi zinakuwepo na zinakabidhiwa kwa wahusika mara baada ya mashindano.

Kwa upande wake Bw.Meshack Fukuta mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019 ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua katika malalamiko yake ambapo ameahidi kufanya juhudi katika Sanaa yake ili kuitangaza nchi vizuri ndani na nje ya nchi pamoja na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
Kifatacho wale bakora maana huu ni uhuni
 
Dah, dogo alipiga show akiwa ametoka kuwekewa drip hospitali, akakamua kweli kweli kumne hakulamba chochote!
Huwa najiona nina roho mbaya kumbe roho yangu sio chafu sana na nikikazana kidogo naweza enda mbinguni.
Unamdhulumuje mtu 50M kirahisi hivyo?
Akina Master j wanajimwambafy tu kumbe pesa hamnamo, walipe.
 
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama Bongo Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019 zawadi yake ya milion 50. View attachment 1412584

==========

Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kuanzia Aprili 08, 2020 kwa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya Bongo Star Search chini ya Mkurugenzi wake Madam Ritha Paulsen kumlipa kiasi cha Shilingi milioni 50 mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa mwaka 2019, Bw.Meshack Fukuta.

Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo leo Jijini Dodoma baada ya kupokea barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa mkononi ambapo Mhe. Naibu Waziri amesisitiza makubaliano yote yalioanishwa kufanyiwa kazi.

“Mimi kama mlezi wa tasnia ya Sanaa ambaye pia nilikua mgeni rasmi siku ya fainali nimesikitishwa sana na malalamiko haya, hivyo naitaka kampuni ya Benchmark kutekeleza ahadi hiyo na wasipofanya hivyo ndani ya muda huo, Serikali haitasita kufungia mashindano hayo”, alisema Mhe.Shonza.

Mhe. Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Benchmark kuhusu malalamiko hayo mbapo Kampuni hiyo ilieleza kuwa imeshindwa kumlipa msanii huyo kutokana na viongozi wa Kampuni iliyodhamini shindano hilo ya Startimes kuwepo nchini China na kushindwa kusafiri kuja nchini kutokana na uwepo wa ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo Mhe.Naibu Waziri ameleeza kuwa Wizara iliwasiliana na uongozi wa Startimes ambao umekiri kuwa umeshalipa fedha kwa Kampuni ya Benchmark tangu mwezi Januari 2020.

Aidha, Mhe.Shonza ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inamtengenezea msanii huyo wimbo bora pamoja na kuufanyia matangazo ya kutosha katika kipindi cha miezi miwili kuanzia leo pamoja na kuwasilisha nakala ya mkataba wa washiriki waliofikia hatua ya kumi bora ndani ya wiki moja kuanzia leo machi 08,2020.

Katia hatua nyingine Mhe.Shonza ameliagiza Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA) kusimamia utaratibu wa uaandaji wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa mikataba kati ya wasanii na wanaondesha mashindano au shughuli yoyote ya sanaa na wasanii pamoja na kuhakikisha ahadi wanazopewa washindi ikiwemo zawadi zinakuwepo na zinakabidhiwa kwa wahusika mara baada ya mashindano.

Kwa upande wake Bw.Meshack Fukuta mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019 ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua katika malalamiko yake ambapo ameahidi kufanya juhudi katika Sanaa yake ili kuitangaza nchi vizuri ndani na nje ya nchi pamoja na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
Nilikuwa najiuliza mbona washindi wa bss maisha yao magumu hawapigi hatua...kumbe huwa anawapiga changa la macho mshenzi sana rita
 
Kitambo sana hapo wamepushana na mshindi ndio maana yanajulikana sasa... Muulize Kala Jeremiah aliambulia nini

Jr[emoji769]
Kumbe huwa anawatumia kuji mekia mkwanja halafu anawapiga changa la macho.mshenzi sana madam
 
Huu mkataba unamnyonya msanii,yaani anaambulia mil 20 cash na mil 30 ahadi hewa eti kupromote kazi yake!!!! Ataishia kurekodiwa studio za hali ya chini au kwa master j ngoma mbovu ndo itakuwa kwa heri,ndo maana wasanii wa bongo star search asilimia 90 wamepotea kusikojulikana!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom