Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Mfumo wetu wote wa utawala na utendaji unahitaji kufanyiwa overhaul reforms! Uwekezaji mkubwa ufanyike kwamza kwenye kubadilisha mindsets za watu. Hivi tulivyo sasa, tukiachwa hivihivi itatuchukua miaka 500 kujikomboa kwenye huu umaskini.Pole sana mkuu, nadhani jibu sahihi ni kubinafsisha taasisi hizi za serikali kwa sekta binafsi.
SUALA LA KATIBA MPYAKila mtu anawaza upigaji tu, yaani vichwa vimejaa ni namna gani fursa ije ili mtu apige.
Huko kwenye ofisi za umma pamejaa mi-ungu watu, kuanzia mfagizi hadi ma-boss!
Badala ya kufanya kazi, watu wamejaa majungu, kuoneana wivu na kuchongeana.
Watu wanafiki kupitiliza. Usoni wanakuchekea kumbe moyoni wamejaza chuki kupindukia.
Watu hawana huruma kabisa na umaskini wa wenzao, yaani hawajali chochote, kila mtu anaangalia maisha yake.
Nimesikitika sana. Kwa namna hii tujajikomboa miaka 500 ijayo!