View attachment 1982420
Kwanza natanguliza hoja kwamba sina chuki yoyote na huyo jamaa kwa sababu hata silijui lolote linalomhusu , bali pia nampongeza kwa kuhamasisha morali ya wachezaji wa Taifa Stars kwa kuhudhuria kwake mechi zao hata zile zinazopigwa nje ya nchi .
Leo ameshinda tuzo ya mhamasishaji bora wa msimu wa Tuzo za ligi iliyopita ya Vodacom (Maajabu) , maana huyu yeye alikuwa Mhamasishaji wa Timu ya Taifa tu , sijui huku kafikaje , ila siyo kesi maana aliwahi hata kuitwa kwenye bunge la Tanzania na kupongezwa .
Swali langu ni hili , huyu jamaa ni nani katika soka la nchi hii , na kwa vile nchi hii haina Uraia pacha amefuata nini ?
Sent from my SM-J500H using
JamiiForums mobile app