Bongo Zozo ni nani na amefuata nini Tanzania?

Bongo Zozo ni nani na amefuata nini Tanzania?

Bongo zozo jamaa anaonesha Ana mapenzi sana na Tanzania namfuatilia tu mtandaoni ila nilitaka kujua kwa undani wake.

Je yeye ni nani na Ana uhusiano upi na Tanzania?
Ameoa na Kuzaana Mwanamke wa Kitanzania, Mkewe ni Mchaga.
Ana Uraia wa nchi gani?
Yeye ni Raia wa Uingereza
Ana nufaika nini kuonyesha mapenzi ya hali ya jua kwa Tanzania?
Ni mapenzi tu aliyonayo kwa Tanzania kama nchi ambayo amewahi kuishi na kubahatika kupata Mke.
Ana Fanya kazi gani maana anazunguka nchi nyingi sana Duniani?
Bongo Zozo ni trader, ni mmoja wa "Early Adopter" wa Bitcoin na Cryptocurrency lakini pia ni Collector wa Coins haswa zile za Zamani. Kwa wenzetu watu aina ya Bongo Zozo wanaitwa "Digital Nomad" hajaajiriwa na mtu yeyote yule, mtaji wake mkubwa ni Laptop yake na uwepo wa mtandao wa internet sehemu yoyote atakayokuwepo kwani shughuli zake za kumuingizia kipato zinahitaji vitu hivyo kama vitendea kazi.

Asante.
 
Sababu una roho mbaya na hii ndio tabia kubwa ya mtu mweusi inayomrudisha nyuma. Kuchukia watu bila sababu. Ni tabia ya kimaskini na laana. Omba Mungu akusaidie uepukane nayo. Ukimchukia Bongo Zozo we unapata nini? Kakuibia chochote?
Okay.
 
Badilika, utapata baraka na mafanikio zaidi ya uliyonayo sasa. Sisi sote ni Binadamu tunahitaji upendo na haki sawa. Analofanya mwingine kama halikuvutii basi liache tu ila usijenge chuki.
Nisicho kipenda toka kwake ni maudhui yake tu!
 
Je yeye ni nani na Ana uhusiano upi na Tanzania?

Ana Uraia wa nchi gani?

Ni muingereza ambaye alizaliwa Zimbabwe, na wazazi wake ambao walikuwa waloezi huko Zimbabwe lakini walirudi kuishi Uingereza wakati Bongozozo akiwa baado mdogo...

Uhusiano wake na Tanzania ulianza pale Bongozozo alipoamua kutaka kuja kuishi Afrika pindi alipomaliza elimu ya chuo, bara alilozaliwa na "asili ya pili ya wazazi wake".

Akaishia kuja Tanzania hatimaye mkoani Iringa sababu ya hali ya hewa yenye ubaridi mwanana, na mwanzo alipanga aishi kwa muda mfupi lakini akajipata anaishi miaka 18 na kuoa mwanamke wa Kitanzania mwenye asili ya Kichaga huko huko Iringa na baadaye akahamia Moshi...

Ana nufaika nini kuonyesha mapenzi ya hali ya jua kwa Tanzania?

Kwa mtu aliyeishi Tanzania kwa miaka 18, mahali ambapo ni ukweni kwake na nchi ya mke wake hivyo it's a no brainer kutokuwa na mapenzi na Tanzania...

Hata watoto wake haswa mtoto wake wa kiume, huwa anawatambulisha kama Watanzania na mwanaye huyo ambaye hushiriki shughuli mbalimbali za kimichezo huwa anaiwakilisha Tanzania kwenye events ambazo sio official haswa riadha...

Ana Fanya kazi gani maana anazunguka nchi nyingi sana Duniani?

Kitaaluma jamaa ni kocha wa mpira wa miguu kwa kusomea. Lakini pia huwa anasema yeye ni youtuber...

Nimeandika kwa mujibu wa mahojiano ambayo nimewahi kumsikiliza na kusoma akielezea historia yake...

Wenye kujua zaidi wataandika zaidi...
 
Back
Top Bottom