Leo nataka niseme kuwa huyu bwana anaitwa bongozozo kuna jambo analifanya na linaonekana na mwelekeo mzuri. Katika video zake nyingi kila anapopata nafasi nzuri huwa anaitangaza sana nchi yetu na vivutio vyake kwa ustadi na weledi siyo ule UJINGA UJINGA wanafanyaga baadhi ya watu wetu maarufu wanapopata platform.
Baadhi ya watu haomaarufu hata taarifa kamili za vivutio vyetu hawana kwaiyo hata wanapoongea kuhusu Tanzania wanaishia kutoeleweka so inakuwa no impact maana hawana communication skills ila kila anapofanya Bongozozo at least you feel and you can see something has been done.
Serikali kama mmejirudhisha kuwa this man is not threat to national security, basi fanyeni nae kazi, mpeni support ya kifedha na platform zaidi ili anachokifanya kilete matokeo zaidi, mpeni vijana kadhaa wa kubadilshana nae mawazo ili awe na team kama itabidi.
Msikilizeni pia nae kama ana mawazo zaidi au maono makubwa zaidi ya hichi anachofanya ili muone namna mnavoweza kuwezesha hizo ndoto ili kama ni kufungua nchi basi ifunguke zaidi maana ni wazi kabisa kuwa Tanzania siyo maarufu kama watu wengi wanavyoweza kudhani kwaiyo kazi ya kuifungua ni endelevu.
Ndio watu wakadanganywa royal tour imeleta watalii mamilioni?
Kwa waliosafiri sana hili linajulikana especially issue ya mlima Kilimajnaro uko wapi wakenya wanajipigia upatu sana upo kwao .
Ukimuuliza mwenyeji akutajie walau nchi tatu za Africa atakutajia South Africa akijitahidi sana Nigeria , wengine wengi tu wanajua Africa ndio nchi sio bara.
Mambo mengine ni ya ajabu kabisa sijui hiyo wizara ya utalii kazi yao ni kugawana tu ela maana hakuna kitu kinafanyika Tanzania haijulikani hata robo tuko.gizani mpaka aibu
Nilikuwa namfuatilia Sana Hapo awali ila nilipokuja kumlinganisha na viongozi na wananchi wa nchi anayon'gan'gana kuitangaza duniani, nafsi ilikata tamaa...
Daah..! pole yake hakika Kama asipolipwa hapa duniani mbinguni atalipwa
Wananchi wamejaa manung'uniko dhidi ya nchi yao itajulikana vipi? Hata watanzania wanaosafiri kwenda nchi za watu wanaona aibu kuitangaza nchi yao iliyojaa Mambo ya aibu.