Bongozozo anaitangaza vizuri Tanzania, Serikali fanyeni naye kazi kama siyo hatarishi

Bongozozo anaitangaza vizuri Tanzania, Serikali fanyeni naye kazi kama siyo hatarishi

Habari wana jf.

Leo nataka niseme kuwa huyu bwana anaitwa bongozozo kuna jambo analifanya na linaonekana na mwelekeo mzuri. Katika video zake nyingi kila anapopata nafasi nzuri huwa anaitangaza sana nchi yetu na vivutio vyake kwa ustadi na weledi siyo ule UJINGA UJINGA wanafanyaga baadhi ya watu wetu maarufu wanapopata platform.

Baadhi ya watu haomaarufu hata taarifa kamili za vivutio vyetu hawana kwaiyo hata wanapoongea kuhusu Tanzania wanaishia kutoeleweka so inakuwa no impact maana hawana communication skills ila kila anapofanya Bongozozo at least you feel and you can see something has been done.

Serikali kama mmejirudhisha kuwa this man is not threat to national security, basi fanyeni nae kazi, mpeni support ya kifedha na platform zaidi ili anachokifanya kilete matokeo zaidi, mpeni vijana kadhaa wa kubadilshana nae mawazo ili awe na team kama itabidi, msikilizeni pia nae kama ana mawazo zaidi au maono makubwa zaidi ya hichi anachofanya ili muone namna mnavoweza kuwezesha hizo ndoto ili kama ni kufungua nchi basi ifunguke zaidi maana ni wazi kabisa kuwa Tanzania siyo maarufu kama watu wengi wanavyoweza kudhani kwaiyo kazi ya kuifungua ni endelevu.

Heri ya mwaka mpya. Nchi iendeleee kufunguliwa

View attachment 2465850
Hilo ni jasusi au linapata kiki kwa kutumia nchi yetu. Kwao, wazungu hawampi fursa mtu mweusi. Kuna kinachoendelea. Ni ukoloni tu wa kawaida ambao hata tapeli kama huyu anaweza kuutumia kujinufaisha na kuwahadaa wadanganyika
 
Hakuna beberu anafanyaga kazi ya bure... tukijiridhisha na usafi na nia ya Bongozozo tutafanya nae kazi.
 
Back
Top Bottom