Boniface Jacob (Boni Yai) apatiwa Dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000

Leo, Jumatatu Oktoba 07.2024 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri/serikali dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.

Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Jambo TV

Pia soma: Serikali yakwamisha tena dhamana ya Boniface Jacob (Boni Yai)
 
Kwani anashtakiwa kwa kosa gani la msingi?
 
Alikua ana Tatizo gani kwani ndrugu zango wadau 🐒
 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa dhamana kwa aliyekuwa Meya wa Ubungo na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob.

Boniface anakabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii.
 
Wenye Akili Kubwa tunajua tu kuwa ilikuwa apatiwe Dhamana hii tokea Wiki iliyopita ila Mamlaka kutoka Juu yenye Nguvu hadi Mahakamani huko ilitaka Kwanza ijihakikishie kama yale Maandamano hayapo kabisa na Usalama ni wa Kutosha ndipo wamwachie kwani angeachiwa Wiki iliyopita huku bado kukiwa na Vuguvugu la Maandamano angeweza kuleta Ushawishi mkubwa ukizingatia Jacob nae ana Nyota ya Kipekee ya Kiushawishi japo Watanzania wengi tunamuangusha kwa ama Uwoga wetu au Upumbavu Tukuka wetu au Uchawa wetu.
 
kwamba kahalifu kamoja kalikokua kanataka kujificha uvunguni mwa IST huku kakipiga makelele kasaidiwe na wenzake waoga kweli kweli kasikamatwe na polisi ni threat for peace?🤣
 
Ofcourse wenye akili wanajua Hana kosa lolote ila tu ni ktk harakati za kujaribu kujisafisha visivyosafishika.
 
Wateja wa mayai watakua wamemiss mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…