Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Hao polisi waje wakosee wamtandike risasi itakua poa sana.Kiongozi unataka watu waishi bila utelezi.Stress za maisha zitusumbue na starehe zetu bado mzibanie nyie kina nani bwani si watu km sisi.Wa tz na sisi uzezeta umezidi hawa km tunaamua kuwachenjia watatuheshimu ww dar inachangamoto kibao una kuja hangaika na dada poa.
 
Hao madada poa yeye mwenyewe mteja. Pale hakuna kiongozi. Namuonaga anapokujaga Iringa jinsi anavyotukana, mtejenya na kuchekacheka na yule Dada Kibonge pale kwa Nelly Samora.
Na stiki yake mdomoni si ndio chimbo lake lile na huku kitwiru anatuuzia kabisa ana duka la pombe Sasa inakuwaje anajifanya mhafidhina hivyo aachage ujinga hyu blaza
 
Kuna polisi mmoja alinikuta nje (parking) ktk moja ya Bar za Sinza, akanifata et unasimama hapa we kibaka.

Nilimwambia maneno machache tu..

"Kama anajimudu anifate". Kilichoendelea Siri yangu, kuna muda inabidi busara ikae pembeni kdg
 
Hawa ndio wateuliwa wetu wamekosa hekima, hawajui kuwa aliyesema usizini ni huyohuyo alisema usiue, usiibe, usiseme uongo kwa hiyo dhambi siyo uzinifu tu acheni kuwadharirisha mama zetu. Kuna mapungufu mengi ya nchi yanayotakiwa kufanyiwa kazi.
 
We Chalamila nilikushauri uachane na hii mambo ya kushindana na nguvu za asili....angalia sasa unapata mitihani kwa damu zisizokuwa na hatia......Mwagito...upulike???
Atupishe apelekwe huko kwenye migogoro ya Mashamba Sumbawanga, Rukwa akafanye ubabe wake huko kwa wale walinzi wa kanisa
 
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

2. Mlinzi waliyemua kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza

3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.

4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)

5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.

5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchukua silaha bunduki aina ya (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.

6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)

7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.

8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.

9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila

10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.

Video za chini zikionyesha polisi hao wanafyatulia watu risasi.

Boniface Jacob - Ex Mayorpolisi
 
Back
Top Bottom