Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kesi ya Boniface AK Mwabukusi kupinga kukatwa kwenye Uchaguzi wa Rais wa Tanganyika Law Society kutolewa hukumu leo pale Mahakama kuu ya Tanzania

Jumaa Mubarak 😃

----

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Julai 26.2024 imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi dhidi ya TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika) ambapo Wakili Mwabukusi alikuwa anapinga maamuzi ya kamati ya rufani kumuengua kugombea nafasi ya Rais wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Mahakama imeridhika na hoja zilizotolewa na upande wa Mwabukusi ambapo sasa rasmi imetengua maamuzi ya kamati ya rufani ya TLS, hivyo kwa sasa Wakili Mwabukusi amerejeshwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS.

Pia soma
 
MWABUKUSI ASHINDA KESI DHIDI YA TLS.

Katika kesi yenye msisimuko mkubwa sana Jaji Butamo Kasuka Philip wa Mahakama Kuu (Masijala Ndogo ya Dar es Salaam) ametengua na kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Rufaa ya TLS na kumfanya Mwabukusi kushinda kesi dhidi ya TLS.

Hivyo, basi Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi ni mgombea rasmi wa nafasi ya Rais wa TLS katika uchaguzi mkuu wa TLS wa mwaka 2024.

Uamuzi huu umetolewa hivi punde.

Credit by Matojo Mushumba Cosatta.
 
uvccm na ccm sasa walivyo sura zao
Screenshot 2024-07-26 090436.png
 
MWABUKUSI ASHINDA KESI DHIDI YA TLS.

Katika kesi yenye msisimuko mkubwa sana Jaji Butamo Kasuka Philip wa Mahakama Kuu (Masijala Ndogo ya Dar es Salaam) ametengua na kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Rufaa ya TLS na kumfanya Mwabukusi kushinda kesi dhidi ya TLS.

Hivyo, basi Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi ni mgombea rasmi wa nafasi ya Rais wa TLS katika uchaguzi mkuu wa TLS wa mwaka 2024.

Uamuzi huu umetolewa hivi punde.

Credit by Matojo Mushumba Cosatta.
Dunia hii ukiwa mnyonge utaonewa sana.

Hongera Adv Kajunjumele
 
Back
Top Bottom