Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

Mteja Hana shida shida ipo kwenye viongozi wa chadema na wafuasi wao kulibebea mbeleko hili suala kama vile ni kesi ya chama. Yani ukipitia mtandaoni ni kama chadema imeshinda kesi.
Basi Chadema ni wapenda haki,ndiyo maana walisimama kidete kuhakikisha hapokwi haki yake, timu ikishinda, mashabiki wake wameshinda,relax
 
Kuna namna wakina Kibatala walikuwa wakitangaza misimao yao kuhusu kumuunga mkono Adv. Mwabukusi arudishwe kama mgombea, but at the same time wanasema hawatampigia kura, nikaona hawa wanajichanganya.

Naamini kile kitendo chao cha kusema hawatampigia kura Adv. Mwabukusi, kiliwafanya watawala waone kumbe Mwabukusi hana madhara kama walivyokuwa wakimhofia, ndio maana sishangai kama Adv. Mwabukusi ameshinda ile kesi yake iliyosikilizwa leo.
Na huyu ndiye Rais wa TLS for sure, atashinda uchaguzi...............

Anapitia figisufigisu kama ambazo Tundu Lissu alizipitia mwaka 2017............

Ziliposhindikana, CCM wakamwinda kwa risasi Ili kummaliza, lakini wapi bwana..........

Hata Mwabukusi anaweza kupitishwa njia hiyohiyo. Lakini hawa watesi wetu wakumbuke tu kuwa SIYO KILA SIKU NI IJUMAA.............!!
 
Mteja Hana shida shida ipo kwenye viongozi wa chadema na wafuasi wao kulibebea mbeleko hili suala kama vile ni kesi ya chama. Yani ukipitia mtandaoni ni kama chadema imeshinda kesi.
Ni kwa sababu Chadema inatetea haki bila kujali itikadi ya kisiasa! Kwa hiyo hujakosea Chadema imeshinda kesi!
 
Tanzania ni republic siyo democracy, yeyote atakayewekwa hapo ujuwe ni mtu anaekubalika na utawala wa juu kisheria.

Tena sisi ni" Presidential Republic", kwa maana nyingine ni "autocracy" hatuna tofauti kubwa na Ufalme.

Nyerere alishawahi kusema hilo kiaina yake, alisema katiba inamfanya awe "dikteta". Hiyo ndiyo maana halisi ya Republic.
 
Go Mwambulukusu go.

Hamnaga mmama ?
Swali la msingi sana.

Tumewahi ku-outsource mmama toka Unguja miaka ya nyuma kidogo, chama cha wanasheria wa Tanganyika kikaongozwa na mmama toka Unguja.

Hatutarajii kitendo hiki cha aibu kuja kurudiwa tena na hawa ndugu wanaojiita mawakili wasomi.
 
Natamani sana kuiona TLS iliyo imara kiweredi kama LSK. Natamani sana TLS kuwa na uongozi ulio makini wenye ushindani wa hoja kama LSK. Mwambukusi ni mtendaji mzuri mwenye uthubutu anayenyoosha kauli na matendo yake. Mwambukusi ni mtendaji zaidi na msimamizi mzuri. Nafasi ya urais wa TLS kwa Mwambukusi nahisi akiupata atakuwa kama gari lililofungwa speed gouverner.... 🤔 Huu ni mtizamo wangu binafsi naweza kukosolewa.
 
Back
Top Bottom