Akizungumza kupitia mtandao wa ClubHouse, Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi, amesema;
Kama kuna walimu wanachanga hela kumchangia @SuluhuSamia kugombea kupitia CCM, sisi wengine tusio na upande ndani ya vyama lakini tunajua Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mkiti CHADEMA kuwa ni mweledi, na anafaa kuwa mgombea Urais kwa nchi hii, kwanini tusiandike maombi kwa CHADEMA tukiwaomba watupe Tundu Lissu ili tumnadi mbele ya Watanzania.
“Mimi ninataka kuuliza swali sitaki hata tuzunguke pembeni, kitu gani kinatuzuia watu wote wenye akili timamu kusema Tundu Lissu @TunduALissu ndiye mgombea wetu atakayeshika bendera kutuongoza sasa, kitu gani kinatuzuia kama siyo ubinafsi? Nani asiyejua kwamba Tundu Lissu ndiye mtu anayefaa kwa nafasi ile? Ni kwa sababu tu ya ubinafsi na biashara.
Mimi nilikuwa ninatarajia kusiwepo chama cha upinzani cha kwenda Zanzibar kule aachiwe ACT na kwa huku Bara aliyejitambua kidogo aachiwe nafasi awe CHADEMA, hao wengine wagawiwe vipande vidogovidogo kujiimarisha.
“Kwenye makundi yote ya kiharakati, yenye akili timamu tuanze kumnadi Tundu Lissu lakini ni ajabu hata CHADEMA @ChademaTz hili hawalioni, wanapiga tu danadana na nyinyi wadau na Wanachadema mpo hapa hamsemi ukweli kuwaambia viongozi wenu"
Mgombea urais wa upinzani anatakiwa walau awe na miezi 22 mpaka 23 ya kujinadi kabla ya tarehe ya uchaguzi.
— Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi.