Pre GE2025 Boniface Mwabukusi: CCM wanamnadi Samia kama mgombea wao, nini kinawazuia Upinzani kumnadi Lissu?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ajikite kufanya kazi ya TLS na ya CDM awaachie CDM.

Kama bosi wa TLS anachopaswa kufanya ni kukemea kampeni kabla ya muda na hata kuchukua hatua za kisheria kama zipo.
Hajasema akiwa Raisi hio , wanamzushia tu kumchafua
 
Unamnadi vipi wakati hujapata ridhaa ya Alwatani Kim Jong Mbowe? Patachimbika
 
Ukiwa kiongozi wa Taasisi yoyote utakachoongea mbele ya hadhira kina reflect msimamo wa taasisi unayoiongoza ndo maana viongozi wa taasisi huwa hawaropoki wanalifahamu hilo.
Tundu Lissu alipokuwa rais wa TLS aliacha siasa na kuongelea siasa?

Any way kwani hata iki reflect, rais na wapambe wake hawajaanza kampeni kweli?
 
Kwahiyo mama Abdul kavunja Sheria na sisi tuingie mtegoni? Mgombea wetu anapatikana Kwa mjibu wa Sheria au tuipindishe Sheria? Halafu hizo Njia nyingine mnazopitisha taarifa zenu ni za watu wachache hazitufikii Kwa wakati bado tupo insta, x, na Facebook
 
We jamaa maneno mengi lakini unashindwa kutambua kuwa MAJIMBO NI SERA YA CHADEMA na kiongozi yeyote atakayepeperusha bendera ya chama cha demokrasia na maendeleo ni lazima aifuate.
CHADEMA NI MBOWE,NA FREEMAN NDIO CHADEMA.
Vinaenda MTAWALIA.
Huna Cha kunifunza bwamdogo!
 
Vyama vikiungana wanaweza kufanya jambo ila ubaya ni kua vyama vingine ni matawi ya chama tawala hawawezi fanikisha hilo.

Na wengine wana uroho wa madaraka mbaya mbovu wanataka wawe wao tu.

Na kingine utofauti wa sera kati ya chama na chama.
 
Kwahiyo mama Abdul kavunja Sheria na sisi tuingie mtegoni? Mgombea wetu anapatikana Kwa mjibu wa Sheria au tuipindishe Sheria? Halafu hizo Njia nyingine mnazopitisha taarifa zenu ni za watu wachache hazitufikii Kwa wakati bado tupo insta, x, na Facebook
Kwa vile taarifa zimekufikia wewe basi utawajuza na wengine
 
Chadema huwa haturudii mgombea mara mbili, safari hii tunaenda na Halima mdee.
 
Akizungumza kupitia mtandao wa ClubHouse, Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi, amesema;

Kama kuna walimu wanachanga hela kumchangia @SuluhuSamia kugombea kupitia CCM, sisi wengine tusio na upande ndani ya vyama lakini tunajua Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mkiti CHADEMA kuwa ni mweledi, na anafaa kuwa mgombea Urais kwa nchi hii, kwanini tusiandike maombi kwa CHADEMA tukiwaomba watupe Tundu Lissu ili tumnadi mbele ya Watanzania.

“Mimi ninataka kuuliza swali sitaki hata tuzunguke pembeni, kitu gani kinatuzuia watu wote wenye akili timamu kusema Tundu Lissu @TunduALissu ndiye mgombea wetu atakayeshika bendera kutuongoza sasa, kitu gani kinatuzuia kama siyo ubinafsi? Nani asiyejua kwamba Tundu Lissu ndiye mtu anayefaa kwa nafasi ile? Ni kwa sababu tu ya ubinafsi na biashara.

Mimi nilikuwa ninatarajia kusiwepo chama cha upinzani cha kwenda Zanzibar kule aachiwe ACT na kwa huku Bara aliyejitambua kidogo aachiwe nafasi awe CHADEMA, hao wengine wagawiwe vipande vidogovidogo kujiimarisha.

“Kwenye makundi yote ya kiharakati, yenye akili timamu tuanze kumnadi Tundu Lissu lakini ni ajabu hata CHADEMA @ChademaTz hili hawalioni, wanapiga tu danadana na nyinyi wadau na Wanachadema mpo hapa hamsemi ukweli kuwaambia viongozi wenu"

Mgombea urais wa upinzani anatakiwa walau awe na miezi 22 mpaka 23 ya kujinadi kabla ya tarehe ya uchaguzi.

— Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi.
Yametimia

The lone wolf is barking rhymes

Mpaka Mseme
 
Huyu rais wa wanasheria anashauri upinzani uvunje Sheria za uchaguzi au anamaanisha nini
 
Back
Top Bottom