Ikiwa zimepita siku 8 tu tangu tukio la wanandoa, Antony Ngaboli na mkewe, Anna Amiri, kukutwa wamekufa kwa kuchinjwa kikatili chumbani kwao, Bonyokwa, kijana ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amekutwa amekufa chumbani kwake mwili ukiwa unaning'inia kwa tafsiri ya kujinyonga au kunyongwa.
Tukio hilo limetokea saa 5 asubuhi ya leo Juni 20, 2025 maeneo ya Bonyokwa-Mwisho wa Lami wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo ameacha barua ambayo haikuwekwa wazi ilikuwa na ujumbe gani na kuna tetesi kwamba, polisi wameichukua.
Ilielezwa kuwa, marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake kwenye nyumba ya familia na alikuwa kijana mwenye tabia ya kawaida.
Difenda la polisi lilifika eneo la tukio kwa ajili ya kuuchukua mwili huo huku baadhi ya akina mama wakifika na mikeka ya kuubebea mwili huo.
Itakumbukwa Juni 12, mwaka huu, mfanyabiashara Antony na mkewe Anna walikutwa chumbani wamekufa kwa kuchinjwa huku vifo vyao vikiacha simulizi tata hadi sasa huku Jeshi la Polisi likisema linaendelea na uchunguzi.
Marehemu hao, walizikwa jana wilayani Mwanga, Kilimanjaro na wameacha watoto watano.
Mashuhuda wamesema hii ni alama ya 'roho ya mauti' kuiandama Bonyokwa wakishauri wakazi wa eneo hilo kumwomba Mungu aepushe vifo zaidi vyenye vyanzo vya aina hiyo.