Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Tangu mwaka umeanza nesoma vitabu kadhaa
To kill a mockingbird
The fault in our star
Everything is fucked
Ego is the enemy-Hiki nimekirudia ni kama bibilia kwangu

Mkuu, kuna kitabu kinaitwa The Fountainhead( Ayn Rand) ambapo mwandishi anadai kuwa ego ndio kisima cha maendeleo ya binadamu. Nahisi kama kutakuwa na mgongano wa mawazo kati ya Ayn Rand na mwandishi wa hicho Ego is The Enemy.

Ayn Rand-RIP(ameandika pia Atlas Shrugged) hakutokea kupendwa na wasomaji wengi kwa sababu ya falsafa yake ya objectivism, ambayo inasemekena kufuatwa na Trump na wafuasi wake.
 
Sasa hard copy ndio nzuri. Tatizo ni umeanza kuangalia ukubwa wa kitabu.
Ungetakiwa usome bila kuangalia.

Upo day ngapi leo?
[SUB]dah kwa kuviangalia vinatishia.[/SUB]

[SUB]the magic nipo day three,nimesita kwanza kuingia day 4 nafanyia kazi haya ya day 1,2 and three.[/SUB]
 
Jinsi unavyosoma ndio unazidi kukipenda,kinaelezea mambo yanayoendelea sasa USA.

Niwe mkweli mwenyewe nilikisoma mara ya kwanza nikaacha,nikarudia tena nikaacha,mara ya tatu ndio nimekimaliza.

Ni kweli mkuu.

Huu ubaguzi wa rangi dhidi ya weusi U S A unaonekena pia kwenye To Kill a Mockingbird.
 
Hicho sijakisoma mkuu,nitajitahidi nikisome,sometimes naona ni vizuri kusoma vitabu viwili vinavyokinzana ili kuweza kuchambua mambo kiundani badala ya tu kuegemea upande mmoja.

Kuna jamaa anaitwa Mark Manson ameandika kitabu titled "The subtle art of not giving a https://jamii.app/JFUserGuide" napenda sana uandishi wake yeye yuko tofauti kabisa na waandishi wengine wa hizi self help books.
 

Kama una soft copy ya hi hiyo The Subtle Art of.......naomba uiweke hapa mkuu.
 
Nimejaribu kufanya kautafiti, inaonyesha hivi vitabu vilianza kuandikwa kwa mfululizo huu...

1. The Secret (Mwaka 2006)

2. The Power (Mwaka 2009)

3. The Magic (Mwaka 2012)

5. Hero (Mwaka 2013)

NB: Sijaanza kusoma ila i think "content" yake haifwati mfululizo huo, ni kama vina jitegemea.
 
Vipo vinne
1.The secret
2.The magic
3.The power
4.The hero
 
Kwa nini yuko tofauti mkuu ?
 
Asante sana kiongozi kwa ufafanuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…