Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Ule uzi wako wa vitabu upo wapi? Nimemaliza kusoma Prisoners of Geography na Shoe dog. Vitabu safi sana. Nataka nipekue kingine.
Huu hapa;


Vitabu vyangu bora vya nyakati zote. Vipi vyako?
 
Shukrani sana
 

Wow! Hongera sana umemaliza haraka, bila shaka hukuweza kuvumilia kupitisha siku bila kusoma hata pages kadhaa hahaha!!

Yes yes zile Romance scenes Ken amejua kututeka [emoji2][emoji2], hasa ile ya kwenye ndege ilinibidi nitafute picha ya Pan American nione haha,

Harry alikua muhuni muhuni sana,

Hivyo vitabu hapana siuzi, nilikua napiga picha nikivipokea au kununua siku ya kwanza kabla sijaanza kusoma.


 
Hivi hizo nguvu za kusoma fiction book huwa mnazitoa wapi? Mimi nilishashindwa kabisa kusoma fiction

fictions zina raha yake, pia zinajenga ubongo maana hakuna picha ni maneno tu so ubongo utakuwa unatengeneza picha na kuSimulate matukio....wataalamu wanasema hilo ni jambo zuri kwa afya ya ubongo.

jaribu kutafuta fiction story book moja fupi yenye maudhui unayopenda uanze kujizoesha taratibu chief,
 
Kitabu Gamba la nyoka cha Kezilahabi.

Hotuba ya mwenyekiti wa kijiji cha Kisole, Ndungu Malima, wakati wa uzinduzi wa bomba la kijiji.

Jinsi alivyoipamba😀😀

"Wazee walisema, mlima usiosikia huungua watu wakiutazama tu....

Wazee wetu walisema kwa kimako, "Mvua inyeshe leo na uyoga upate leo?" tutasubiri matunda ya juhudi yetu, umoja wetu na nguvu zetu, kwani nyoka mwenda pole huvuka maji yaendayo kasi. Ndama huzaliwa na masikio, pembe huota baadaye."
 
Thank you, Mr Miller.
You see, the book was really interesting. It took me about 3-4days(maybe?)to finish. Nilikuwa nasoma a few chapters a day on my daily commute.

Same here, nili-google nione hiyo flying boat ilivyokuwa. Na nikagoogle hadi honeymoon suite ya Nancy, Lol.
 
Hivi nadharia ni tofauti na fact?
Mwalimu wangu Mubarridi zile unasoma ni Nadharia?
Neno "fact" katika tafsiri ya kiswahili isiyo rasmi tunaweza kusema ni UKWELI ,ambapo neno "theory " ni Nadharia ,
Kwahiyo ,,fact ni tofauti kabisa na nadharia ambayo ni theory ,,


Fact; is a statement or assertation of verified information about something that is the case or has happened and its truthness can be proved beyond any doubt and it occurs in the real world eg,,an example of a fact is that the world is Round, WHEREAS,

Theory is a supposition or a system of ideas intended to explain something especially one based on General principle independent of the things to be explained.
Eg , Darwins's theory of evolution
 
Nasoma kitabu hiki kwa sasa.

Ni kitabu cha mwaka 2008 [sijui kwanini nilikiweka kwenye orodha ya kukisoma muda wote huo], kimeandikwa na mchumi wa kikorea na mhadhiri huko Cambridge University.

Ujumbe uliopo kwenye kitabu hiki ni wa kupinga sera za taasisi za kimataifa za kifedha ambazo zinazitaka nchi masikini kuwa na sera biashara na soko huria, kushusha fedha zao, na kuruhusu uhuru wa mitaji kuingia nchini mwao ili ziweze kupiga hatua za Maendeleo ya viwanda (kiuchumi). Chang anarejea historia za chumi za nchi kama Uingereza na Marekani—viranja wa sera za uchumi huru—kuwa viwanda na uchumi wao haukujengwa kwa sera hizo, bali kwa kulinda viwanda vichanga, kuvipa ruzuku, kuweka kodi/ushuru mkubwa kwa bidhaa/rasilimali za kigeni, kuzipa hodhi ya kibiashara—kwa lengo moja tu ili viweze kukua na kuwa na uchumi imara. Baada ya kufanikiwa kuwa na uchumi imara ndipo mataifa haya yalianza kukumbatia sera za biashara huru. Hivyo kimsingi hoja yake—kwa ushahidi wa takwimu na historia—ni kuwa uchumi wa nchi haujengwi kwa sera za soko huru bali kwa sera za kulinda wazalishaji wa ndani ili waweze kusimama na kuwa washindani.

Kwa 20% nilizofika, naweza kukushawishi ukisome kitabu hiki. Hata mambumbu wa uchumi, tunaweza kuelewa lugha yake.
 
Thank you for breaking it down for me.
 
Wow, kazi nzuri sana.
Ambao tumeshawishika na tunaki add kwenye "must read "hiki hapa,
 

Attachments

Nadharia ni tofauti na fact. Kadhalika kuna mdau msome hapo juu ameelezea vizuri tofauti baina ya tamko "Nadharia" na "Fact(Uhalisia)".

Mimi huwa nasoma "Fact(Uhalisia)" mwanafunzi wangu.
Asante mwalimu wangu. Ila nyingine zile sio fact huwa ni conspiracy. Ila sawa nimeelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…