Nasoma kitabu hiki kwa sasa.
Ni kitabu cha mwaka 2008 [sijui kwanini nilikiweka kwenye orodha ya kukisoma muda wote huo], kimeandikwa na mchumi wa kikorea na mhadhiri huko Cambridge University.
Ujumbe uliopo kwenye kitabu hiki ni wa kupinga sera za taasisi za kimataifa za kifedha ambazo zinazitaka nchi masikini kuwa na sera biashara na soko huria, kushusha fedha zao, na kuruhusu uhuru wa mitaji kuingia nchini mwao ili ziweze kupiga hatua za Maendeleo ya viwanda (kiuchumi). Chang anarejea historia za chumi za nchi kama Uingereza na Marekani—viranja wa sera za uchumi huru—kuwa viwanda na uchumi wao haukujengwa kwa sera hizo, bali kwa kulinda viwanda vichanga, kuvipa ruzuku, kuweka kodi/ushuru mkubwa kwa bidhaa/rasilimali za kigeni, kuzipa hodhi ya kibiashara—kwa lengo moja tu ili viweze kukua na kuwa na uchumi imara. Baada ya kufanikiwa kuwa na uchumi imara ndipo mataifa haya yalianza kukumbatia sera za biashara huru. Hivyo kimsingi hoja yake—kwa ushahidi wa takwimu na historia—ni kuwa uchumi wa nchi haujengwi kwa sera za soko huru bali kwa sera za kulinda wazalishaji wa ndani ili waweze kusimama na kuwa washindani.
Kwa 20% nilizofika, naweza kukushawishi ukisome kitabu hiki. Hata mambumbu wa uchumi, tunaweza kuelewa lugha yake.
View attachment 1948623