Asante sana.
Nadhani ni mipangilio tu ya mambo yako na muda wako, kwa wakazi wa Dar tunaotumia daladala kila siku kwenda kwenye majukumu yetu tunatumia zaidi ya saa moja kwenye foleni, muda huo unaweza kuutumia na kitabu vizuri tu.
Saa moja au nusu saa kabla ya muda wako wa kulala unaweza pia kujiwekea lengo walau usome kurasa 20 za kitabu kila siku muda huo, taratibu unajikuta ukifikia lengo.
Nimepunguza sana pia muda wa kutazama TV programs na series na muda ninaookoa hapo nauhamishia kwenye usomaji.
Episode moja ya series si chini ya nusu saa, kwa msomaji mzuri muda huo huo unaweza kuwa umesoma kurasa zako 20 vizuri tu.