1.kama ulisoma my last quote niliyokuquote niliongelea suala la nyumba ( kumiliki nyumba) . una kumbuka?
Ni kweli nyumba unaweza isiwe investment na literally alikuwa anasema ni bora kupanga na kuwekeza kwenye real estate (RE).
Tuje kwenye uhalisia nikutolee mfano wewe, kama una familia yako mke na watoto. Maana yake ukisema usijenge ili kupanga nyumba nzuri itakuhitaji kulipa kodi ya shilingi ngapi kwa mwezi? Kwa mwaka jee? Haitoshi kununua au kujenga nyumba?
Okay alisema kwamba kumiliki nyumba ni expenses , itahitaji ulipe maintainance cost. Lakini kwani gharama ya maintainance ni shilingi ngapi na inafanyika Mara ngapi baada ya miaka mingapi?
Expences kama bills za maji , umeme hizo hazikwepeki kwa sababu hata uki rent a house lazima ulipe.
Nilikwambia kilichotokea kwa watu ambao walikuwa wanachota kila kitu ambacho kiyosaki anasema, bila kuchuja na kujua sio vyote vina work kwa kila mtu na kwa maisha ya kitanzania au ya kiafrika, Leo wamefilisika kwenye miradi waliokuwa wamewekeza, na nyumba za kuishi hawana zaidi sana wameishia kurudi vijijini baada ya kushindwa kumudu hata kodi.
Kwangu Mimi naona kumiliki nyumba unasave cost nyingi sana tofauti na ukipanga nyumba. Na ninaweza kumshairi Mtu kwa proper utilization za hela ni bora ajenge nyumba, halafu aanze kusave excess money ambazo angekuwa anapigwa kwenye hizo za kupanga.
2.Issue ya Elimu. Huwa anaishusha hadhi sana elimu na kufanya vijana wengi wasitamani kusoma. Ana msemo mmoja kwamba wenye C wamewaajiri wenye A. Yaani kwa maana nyingine ni kwamba wasomi wameajiriwa na ambao hawajasoma. Kwahiyo kwa kifupi haoni umuhimu wa shule. Na vijana siku hizi wameshikilia huo msemo sana tena baada ya kushindwa kufanya vizuri shuleni.
Lakini wanashindwa kujiuliza bila shule wangeweza kweli kusoma hata this rich dad and poor dad? Bila shule wa naweza kuelewa concept zote alizoziandika kwenye kitabu? Proper management ya fedha inahitaji pia elimu. Well na kama kweli shule haina maana kwanini huyo aliyefeli inabidi amwajiri msomi ili afanikishe mipango yake?.
NDIO MAANA NIKASEMA KIMEKAA KUTOA FARAJA BADALA YA NJIA SAHIHI.
NB, kumbuka haya ni mawazo yangu yanaweza kuwa sahihi au sio sahihi.
Ok, Paula, sasa tunaenda vizuri..
Moja ya vitu vilivyosababisha kitabu chake kikataliwe hadi akichapishe mwenyewe ni hoja tatu,
1)Saving money is foolish.
2)Dont work for money na ya tatu ni uliyosema
3)Your house is not an asset, tuijadili',
Nafikiri unakubaliana na definition yake ya asset na liability, na unakubali pia kwamba ili utajirike unatakiwa kununua asset badala ya liability...
Kwamba, badala ya kununua nyumba uishi wewe, nunua nyumba upangishe, hesabu inatakiwa kuwa kwamba, gharama utakayokuwa unatumia ulikopanga iwe ndogo kuliko pesa unayoingiza ulikopangisha, ina maana utapokea rent ambayo itacover pango lako na kubakisha, hiyo unayobakisha ndio profit..
Sijui kama ninaeleweka, inambna hiyo nyumba ungeishi mwenyewe, usingeingiza kitu na ungeilipia kodi na maintainance, tayari ingekuwa liability, ingekuwa ni expenditure, badala ya income.
Mtu mwenye nyumba ya kupangisha anafilisikaje ili hali inamwingia pesa kila mwezi?
Mimi nadhani mwenye nyumba ya kuishi ndio anafilisika maana haiingizi na inamgharimu pesa..
Kwa mfano, watu hawa wawili wakipoteza kazi, mmoja ana nyumba ya kupangisha mwingine hana, nani atasurvive?
Tofauti iliyopo kati ya asset na liability, When you lose your job an asset will feed you, but a liability will eat you!
Suala la elimu Kiyosaki halipingi, lakini anasema elimu ya darasani(formal education)ina mapungufu, inatoa
1)Academic education
2)Professional education
Lakini haitoi
3)Financial education.
Ninadhani yuko sahihi, wewe unaonaje Paula?