Hata mimi sijakisoma ila nimeona muvi nyingi zinazohusu hichi kitabu ndio nikashawishika nikitafute..
Vipi J.R.R.Tolkien umewahi kumsoma kazi zake? Kama jubu ni ndio unaona nani ni bora kati yake na G.R.R Martin
?
Cc
James comey
J R R Tolkien, Lord of the Rings (1-3)
na G R R Martin, A Song of Ice and Fire(1-7).
Zote ni epic novels zinazosimulia vita ya wema dhidi ya uovu.
Tofauti moja ni kuwa ndani ya Lord of the Rings ni rahisi kuwajua wema mapema( ukimwacha Saruman the White).
Kwenye A Song of Ice and Fire ambako kuna wahusika lukuki sio rahisi kuwabaini wema na wabaya kati ya wahusika wakuu ingawa kuna utakaowachukia mwanzoni na kutamani washindwe.
Setting ya nyakati pia ni tofauti, ya Lords of the Rings ikiwa ya kubuni moja kwa moja huku ile A Song... ikishabihiana na zile vita zilizoibua mataifa ya Ulaya ya zama hizi( e.g UK etc)
Pia characters wa Tolkien (mf. Hobbits na elves) na events zao ni supernatural zaidi wakati kwenye A Song of Ice and Fire kuna mchanganyiko wa matukio na wahusika katika pande zote mbili.
Katika A Song of Ice and Fire kumejaa ukatili usiomithilika. Ni kama vile G R R Martin ana-potray kiwango cha uovu ndani ya binadamu na matumizi ya mabavu na kuvishabikia wakati J R R Tolkien aki- potray watu wema waliolazimika kuingia vitani ili kupinga uovu.
Ni yupi bora kati ya Tolkien na Martin? Nadhani hii itategemea uonjo(taste) ya msomaji. Wote wawili wameandika riwaya zinazovutia sana.
Kwa mtazamo wa kiutu, Tolkien ni mtunzi bora sana ukimlinganisha na Martin.